Zlatan Ibrahimovic akalia kuti kavi Man United

Muktasari:

  • Kocha Jose Mourinho huenda akamuuza mapema zaidi mshambuliaji huyo kutokanana kuumia tena.

Mshambuliaji wa Manchester United, Zlatan Ibrahimovic ameingia kwenye anga mabaya za Jose Mourinho kutokana na kukabiliwa na majeraha jambo ambalo huenda akawekwa sokoni haraka.

Ibrahimovic amekubwa na majeraha ambayo inaonekana yatamuweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

Mshambuliaji huyo aliyetamba msimu uliopitia, alipambana kwa takribani miezi saba ili kuhakikisha anarejea kwenye kiwango chake lakini majeraha yanaonekana kuendelea kumtesa.

Awali, Ibrahimovic aliumia kwenye mechi ya Ligi ya Europa hatua ya robo fainali wakati Manchester United ilipokutana na Anderlecht msimu uliopita.

Mchezaji huyo alirejea Novemba 18 uwanjani akianzia benchi na timu yake ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 didhi ya Newcastle.