Madrid, Man United zakubaliana kuhusu De Gea

REAL Madrid inasemekana imefikia makubaliano na Manchester United kumnunua kipa namba moja wa wababe hao wa Old Trafford, David de Gea kwa dau la Euro 100 milioni katika dirisha kubwa lijalo la majira ya joto baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia.

Real Madrid imejaribu kumrudisha nyumbani kipa huyo wa zamani wa Atletico Madrid kwa miaka mingi lakini inasemekana sasa imefikia makubaliano maalumu na Manchester United baada ya kipa huyo kuonyesha nia ya kurudi nyumbani.

Wakala wa De Gea, Jorge Mendes ametumia wiki kadhaa kukamilisha dili hilo na inasemekana kwa sasa kila kitu kipo sawa na Real Madrid imefanikiwa kumpata mtu wake huku ikikaribia kuachana na kipa wake wa sasa, Keylor Navas.