Ligi ya Wanawake yatimua vumbi Mwanza

Monday September 11 2017

 

By Saddam Sadick

Mwanza. Nyanguge Combine imeanza vyema mashindano ya Ligi ya Wanawake Mkoa wa Mwanza kwa kuichapa JB Fc mabao 4-2.

Mchezo huo umepigwa hii leo kwenye Uwanja wa Nyamagana ukiwa ni wa kwanza kwenye ligi hiyo inayoshirikisha timu tano.

JB ndio walianza kufunga mabao kupitia kwa Reka Joseph dakika ya 18 na Neema Method dakika ya 32.

Nyanguge Combine walisawazisha mabao hayo kupitia kwa Paulina Cosmas dakika ya 29, Mchina Abel dakika ya 40 na Samira Method kuongeza la tatu dakika ya 67 kisha Aneth Makoye kuhitimisha karamu ya mabao kwa kuifungia bao la nne dakika ya 79.