Ishu ya Lulu yamtoa Mama Kanumba

Muktasari:

  • Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba, mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba. Jana Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje, amethibitisha kuwa Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

STAA wa Bongo Movie, Elizabeth Michael (Lulu) ndio hivyo amebadilishiwa kifungo na sasa atatumikia adhabu yake akiwa nje, lakini ishu hiyo imemuibua mama mmoja.

Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba, mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba. Jana Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje, amethibitisha kuwa Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

Lakini, ishu hiyo ikamuibua mama wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa ambaye ameeleza kushtushwa na kuumizwa na uamuzi huo. “Imenilazimu kwenda kanisani kufanya maombi ili kuokoa afya yangu, ninahitaji faraja kwa na haki ya mwanangu, lakini kwa kuwa imeamuliwa hivyo sina cha kufanya,” alisema mama Kanumba.