'Inshu' ya Mama Diamond na Mobeto ngoma nzito

Muktasari:

Esma amezungumzia sakata hilo kwani tangu liibuke yeye na mama yake wamekuwa kama watu wa kurusha vijembe katika akaunti zao za Insragram kupitia picha za Wema Sepetu.

Dar es Salaam: Kitendo cha mama mzazi wa staa wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Plutnumz’ anayeitwa, Sanura Kassim 'Bi Sandra' kumpa kichapo mwanamitindo, Hamisa Mobeto na kukiri katika gazeti moja hapa Bongo, dada wa mwanamuziki huyo, Esma Plutnumz amefunguka.

Esma amezungumzia sakata hilo kwani tangu liibuke yeye na mama yake wamekuwa kama watu wa kurusha vijembe katika akaunti zao za Insragram kupitia picha za Wema Sepetu.

Na baadhi ya vijembe hivyo, Esma aliandika, Wema ni Wifi wa Dunia na mama yake akiongeza kwa kumsifia mrembo huyo wa Bongo Movie kuwa amependeza na anafaa kuolewa.

Esma amezungumza na MCL  Digital na kusema, habari za Mama Diamond kumpa kichapo mwanamitindo, Hamisa Mobeto hana uhakika nazo na kwa mara ya kwanza amezisoma katika mtandao wa Instagram baada ya watu 'kumtagi'.

Amesema: "Mie simtupii vijembe mtu, kumwita Wema wifi sio kitu kigeni kwani alishawahi kuwa wifi yangu, ila mambo ya Hamisa na mama mimi siyajui, unishirikishe. Mambo ya mama na Hamisa wamalizane wao wenyewe."

Hata hivyo Esma amekana mama Diamond na Diamond wamejibizana kisa kupigwa kwa Hamisa na ndiyo maana Mama Diamond hakuja katika Uzinduzi.

Hamisa na mama Diamond wameingia katika bifu kali kwa madai ya Mama Diamond hataki Hamisa akanyage nyumbani kwake Madale kisa anamtuhumu alimwitia watangazaji wa kipindi cha Shilawadu, wakapigwe picha wakati wanaenda Hospitali kumwona Hamisa akiwa amejifungua.