Heri Morris anavyotesa Mbagala Kuu! Acha

Muktasari:

  • Hivi unajua kuwa jamaa ana shavu la maana kule maeneo ya Mbagala? Ni mjumbe wa Serikali ya mtaa wa Mbagala Kuu Kaskazini.

UNAMKUMBUKA yule straika aliyetesa sana kwa mabao alipokuwa na kikosi cha Yanga mwaka 2002-07? Anaitwa Heri Morris Ng’onye na alijiunga na Yanga akitokea Prisons?

Hivi unajua kuwa jamaa ana shavu la maana kule maeneo ya Mbagala? Ni mjumbe wa Serikali ya mtaa wa Mbagala Kuu Kaskazini.

Sasa ukimkuta katika maeneo yake lazima umkubali kutokana na shughuli anayoifanya, jamaa anapiga kazi balaa mara kamhudumia huyu, yule ili mradi tu mambo yake yaende sawa, yaani ni kama vile alivyokuwa kipindi kile alipokuwa na vikosi vya Yanga na Tanzania Prisons.

Ni kama anavyoonekana kwenye picha utamkubali tu. Morris aliacha soka kutokana na kuandamwa na majeruhi.