Chelsea kutesti mastaa wake Australia

Muktasari:

  • Kikosi hicho ambacho kimesheheni mastaa wengi chipukizi, kinatarajia kuanza kuonyesha makali yake kwenye mechi hizo za kirafiki ili kumshawishi kocha huyo mpya.

Kocha huyo raia wa Italia alichukua mikoba ya Antonio Conte ambaye ametimuliwa baada ya kushindwa kutetea taji lao la ubingwa msimu uliopita.

Blues wanajiandaa na michezo ya kirafiki itakayopigwa Australia, Ufaransa na Iceland katika msimu huu wa kiangazi.

Kikosi hicho ambacho kimesheheni mastaa wengi chipukizi, kinatarajia kuanza kuonyesha makali yake kwenye mechi hizo za kirafiki ili kumshawishi kocha huyo mpya.

Hata hivyo tayari kocha huyo mpya ameanza kukinoa kikosi hicho tangu atue kwenye dimba la Stamford Bridge.

Mazoezi hayo yalifanyika kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea wa Cobham kabla ya kukwea pipa kuelekea Australia ambako watacheza na Klabu ya Perth inayoshoriki Ligi Kuu ya nchini humo maaraufu A-League siku ya Jumatatu.