Buku saba tu, unamuona Bocco, Ajib

Muktasari:

Viingilio vilivyotangazwa na TFF sio vya kutisha sana na kwamba, kama unataka kushughudia mtanange huo basi utalipia Sh7,000 ambacho ndio cha chini kabisa. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkubvwa kutokana na ukweli kwamba, ndio utatoa taswira ya ubingwa msimu huu, wakati Simba ikiwa ndio vinara wakiwa na pointi 58 na mabao 55 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 47 katika michezo 22.

KUMEKUCHA! Ule mtanange wa watani wa jadi, Yanga na Simba au Kariakoo Derby ndio imefika inaambiwa. Yanga na Simba zitashuka dimbani Aprili 29 na tayari Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo.

Viingilio vilivyotangazwa na TFF sio vya kutisha sana na kwamba, kama unataka kushughudia mtanange huo basi utalipia Sh7,000 ambacho ndio cha chini kabisa. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani mkubvwa kutokana na ukweli kwamba, ndio utatoa taswira ya ubingwa msimu huu, wakati Simba ikiwa ndio vinara wakiwa na pointi 58 na mabao 55 huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 47 katika michezo 22.

Kwa mujibu wa TFF mpango mzima wa viliingilio uko hivi. Jukwaa la VIP A itakuwa Sh 30, 000, VIP B na C Sh 20,000 wakati upande wa mzunguko itakuwa Sh 7000. Katika hatua nyingine, TFF imezitaka klabu zote kuwa makini na mikataba wanayoingia kati ya wachezaji pamoja na makocha. Msemaji wa TFF, Clifford Ndimbo alisema jana kuwa kama klabu itashindwa kuingia mikataba inayoeleweka na makocha na wachezaji hawatasita kuzikata fedha ili kufidia madai ya watumishi wao hao.

Alisema hatua hiyo inalenga kuondoa malalamiko ya wachezaji na makocha dhidi ya klabu hivyo, TFF haitasita kuchukua hatua kama itabaini kuwepo na ubabaishaji.