Antonio Conte ashauri vigogo wa Chelsea kubana matumizi

Muktasari:

  • Conte alitoa tahadhari hiyo kutokana na klabu hiyo kutumia zaidi ya Pauni 140 milioni kusajili wachezaji mwaka 2015.

London, England. Kocha wa Chelsea amewashauri mabosi zake kuwa wanapaswa kuweka akiba kwa ajili ya usajili ujao.

Conte alitoa tahadhari hiyo kutokana na klabu hiyo kutumia zaidi ya Pauni 140 milioni kusajili wachezaji mwaka 2015.

Kocha huyo alitoa angalizo hilo kutokana na kuwaeleza kwamba msimu huu huenda ukawa mgumu zaidi kwa sababu klabu yake inatakiwa kutetea taji la ubingwa wa England.

Alisema jambo kama hilo liliwahi kuwatokea Manchester City ambao walitumia takribani Pauni 200 milioni kwa usajili ambao haukuwa na matunda kwao.