Antonio Conte? Hapana aje Allegri

Muktasari:

Conte amekuwa akihusishwa kuchukua mikoba ya Unai Emery huko PSG, lakini Roche atapenda zaidi kama timu hiyo itamchukua Kocha wa Juventus, Max Allegri.

PARIS, UFARANSA

BEKI wa zamani wa PSG, Alain Roche ameitaka klabu yake hiyo ya zamani kuachana na Kocha wa Chelsea, Antonio Conte.

Conte amekuwa akihusishwa kuchukua mikoba ya Unai Emery huko PSG, lakini Roche atapenda zaidi kama timu hiyo itamchukua Kocha wa Juventus, Max Allegri.

Roche alisema: “Ana staili yake hivi, Emery. Lakini, lazima tucheki kocha mwenye rekodi, uwezo pia wa kufundisha klabu kubwa za Ulaya.

“Conte? Huyo mtu hapana. Hii siyo vita tofauti, lakini mimi si shabiki wake. Siku zote anapiga kelele tu, nampendelea mtu kama Allegri yupo vizuri sana. Ni mtu ambaye anaweza kuweka mipango yake kwenye timu bila ya kuwa na tatizo lolote kwa wachezaji kutokana na uwezo wake wa kusimamia tabia zao.

“Sio tu mataji ya Italia, amefika nusu fainali mbili na fainali moja ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Ana mkataba wa mwaka mmoja tu, hivyo ni wakati mwafaka kumfuata.”