Alaa Kumbe!

Muktasari:

  • Yanga ndiyo vinara na hawakamatiki kabisa katika ufalme huo, wakiwa wamechukua mara 27, Simba mara 18 , ambao wao kama Simba wamechukua mara 16 pamoja na mara mbili wakati inaitwa Sunderland mwaka 1965 na 1966.

KAMA ulikuwa hujui ni, Ligi Kuu kwa mara ya kwanza ilianza mwaka 1965 na tangu msimu huo, mpaka sasa ni timu tisa tu ndiyo zimeshafanikiwa kutwaa ubingwa huo.

Yanga ndiyo vinara na hawakamatiki kabisa katika ufalme huo, wakiwa wamechukua mara 27, Simba mara 18 , ambao wao kama Simba wamechukua mara 16 pamoja na mara mbili wakati inaitwa Sunderland mwaka 1965 na 1966.

Mtibwa Sugar maarufu kama Wanatamtam wanashika nafasi ya tatu baada ya kuchukua mara mbili msimu wa mwaka 1999 na 2000 na himu nyingine zote ni mara moja tu.

Azam FC waliutwaa msimu wa mwaka 2013-2014, Coastal Union 1988, Tukuyu 1986, Pan African 1982, Mseto 1975 na Cosmal Politan 1967.