Sep 5, 2010, 12:42 pm TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-07-27 13:40:00
Ray:Wanawake charukeni
Msanii Ray
Na Julieth Kulangwa
MWIGIZAJI mkongwe ,Vincent Kigosi maarufu kama Ray amesema uhusiano wa kimapenzi wa wasanii mbalimbali wa filamu haumaniishi kuwa tasnia hiyo imegubikwa na wingu la rushwa za ngono na amewaambia wasi chana wakikumbana na hali hiyo wacharuke.

Ray anasema kama mashabiki wanafahamu uhusiano wa kimapenzi baina ya waigizaji au muongozaji na mwigizaji ni uhusiano uliosababishwa na hisia za kimapenzi kama watu wengine.

"Mwigizaji au mwongozaji wanapokuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi haimaanishi kuwa wawili hao wanafanya hivyo kama biashara fulani, ni hisia tu za kimapenzi zinazoweza kuingia kwenye moyo wa binadamu yeyote bila kutarajia,"anasema muigizaji huyo.

"Nashangaa kwanini wanahusisha uhusiano wa wasanii na rushwa ya ngono, jamani si mnaona watu walivyo na mvuto, kuna wakati wote wanakuta wanashindwa kujizuia na kuzama kwenye mapenzi," anasema Ray huku akicheka.

Ray anasema kila mtu anaweza kuanguka kwenye penzi na mtu aliye karibu na maisha yake ya kila siku na hii ndio sababu kubwa.

"Hata wewe mwandishi niambie, ni waandishi wangapi wana uhusiano huko kwenye tasnia yenu, najua pia huko inaitwa rushwa hasa kwa wanawake kutaka msaada lakini ukweli ni kwamba ndio watu wanaozunguka huko.

"Asilimia kubwa ya watu unaokutana nao ndio rahisi kuanzisha uhusiano, kwa hiyo hiki kinachotokea hapa si rushwa ni mapenzi tu ya wasanii wenyewe," anasema Ray muigizaji huyo wa aliyeigiza filamu bomba ya 'Fake Pastor'.

Hata hivyo Ray amekiri kuwa inawezekana wakawepo watu wenye 'vijitabia' hivyo na anaona kuwa ni wababaishaji walioingia kwenye fani hiyo kama mamluki.

"Siwezi kusema tasnia nzima ina watu safi, sisi si malaika na hata linapokuwepo kundi la watu wema ibilisi hakosi kuingia kati ili kuharibu.

Inawezekana watu wenye tabia hizi wakawepo lakini kusema ukweli ukiwachunguza unaweza kuwaona, kwanza hawawezi kufanikiwa kwenye kazi zao.

"Kama unaamua kumpa nafasi msichana au mvulana kwa sababu zako binafsi, nina hakika kazi hiyo haiwezi kuwa nzuri, ndio maana nasema huwezi fika mbali ukiwa na tabia hii.
"Kwa sababu kama kazi itakuwa mbaya inamaana haitafanya vizuri sokoni na huo ndio mwanzo wa kujimaliza, binafsi sifanyi upuuzi huo kwa sababu nina malengo makubwa," anasema Ray.

Ray, ambaye yuko katika hatua za mwisho za kukamilisha filamu yake ya 'Bed Rest' amewaasa wasanii chipukizi kutohadaika na ahadi za watayarishaji wa filamu uchwara na badala yake wazitafute nafasi kwa jasho.

"Kama wewe ni msanii mwenye kipaji na una nia hasa ya kuonyesha kipaji chako, mimi huwa natoa nafasi hizo , nione ofisini kwangu, RJ Company zilizopo Sinza unaweza kupata nafasi ya kuonyesha kipaji chako.

"Ukikutana na mtayarishaji wa filamu akakutaka kimapenzi, usikasirike na kumtukana, uchukulie kama mtihani wa kuyafikia mafanikio, ondoka na katafute nafasi mahali pengine, amini ipo sehemu Mungu amekuandikia, kutoa rushwa ya aina yoyote ni sawa na kudhihaki kipaji ulichopewa na Mwenyezi Mungu."
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4414