Sep 5, 2010, 12:00 pm TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-07-27 13:39:00
TFF ijipange na uchezeshaji duni
MOJA ya malalamiko ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita ilikuwa kiwango cha chini cha uchezeshaji wa waamuzi.

Hata hivyo, kwa sasa limedhihirika ni tatizo la kimataifa kutokana na makosa mengi yaliyotokea kwenye fainali zilizopita za Kombe la Dunia.

Kulikuwa kuna maamuzi mengi yenye utata kwa mfano kitendo cha Harry Kewell kutolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mechi kati ya Australia na Ghana.

Kiungo wa England, Frank Lampard kujikuta bao lake likikataliwa wakati wa mechi dhidi ya Ujerumani licha ya ukweli kuwa mpira ulivuka mstari.

Mechi baina ya Mexico na Argentina, mwamuzi aliruhusu bao la Carlos Tevez licha ya kuwa dhahiri alikuwa kuotea.
Makosa yalikuwa mengi kiasi cha kufanya sasa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kufikiria matumizi ya teknolojia ya video kwenye mashindano yake.
Hata hivyo, pamoja na kukabiliwa na shinikizo hilo bado Fifa, imepiga danadana suala hilo kwani haijapeleka ajenda hiyo kwenye vikao vya Bodi ya Kimataifa ya Usimamizi wa Soka (IFAB).
Watu wanaodai teknolojia wanashangazwa na hatua ya Fifa kusita wakati michezo kama rugby, tenisi na riadha wanatumia picha za televisheni katika maamuzi yao.
Kwa Watanzania wanaofuatilia mchezo wa riadha watakumbuka jinsi picha za televisheni zilivyoamua mshindi wa mbio za marathoni za Boston mwaka 1988.
Waandaaji wa mbio hizo walimpa ushindi Ibrahim Hussein Kipkemboi baada ya picha za televisheni kuonyesha alimzidi kwa sekunde moja tu Juma Ikangaa wa Tanzania.
Ni wazi kuwa Fifa inasita kutumia teknolojia kwa kufahamu kuwa mchezo wenyewe unachezwa dunia nzima na kuna mataifa masikini yatakayoshindwa kutumia mfumo huo.
Kwa mfano kwa nchi za Ulaya na zile za Asia halitakuwa tatizo kwa sababu nchi hizo zimepiga hatua kwenye masuala ya sayansi ya teknolojia.
Hata hivyo, kutokana na hali iliyojitokeza Afrika Kusini, Shirikisho la Soka la Ulaya (Uefa) limeamua kujaribu kutumia waamuzi watano kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Shirikisho la soka Tanzania (TFF) nalo linatakiwa kuanza maandalizi ya kushughulikia tatizo hilo kabla ya ligi kuanza.
Kila mwaka kumekuwa kuna kawaida ya waamuzi kupewa mitihani (Cooper Test) lakini haijaonyesha kuwa na tija kwa sababu sasa waamuzi wetu hawaitwi tena kwenye michuano mikubwa ya kimataifa.
Tanzania haikuwa na mwamuzi kwenye Kombe la Kagame, mwaka huu, Kombe la Mataifa ya Afrika na hata zile za Kombe la Dunia.
Tofauti na miaka ya nyuma, ambayo Tanzania ilitoa waamuzi wazuri kama Gratian Matovu, Mshindo Mkeyenge, Zuberi Bundala, Mussa Lyaunga, Hafidh Ally, Abdalla Rajab na wengineo.
Kuna haja kwa TFF kuimarisha mafunzo kwa waamuzi wetu na pia kitu kingine cha kuangalia ni posho zao kwani ni ndogo kiasi cha kuwa hazivutii wasomi.
Kupandisha kiwango cha posho za waamuzi pia kutasaidia kupunguza malalamiko ya rushwa yaliyosababisha waamuzi kadhaa kuadhibiwa.
Ndio maana tunategemea TFF itaangalia kwa mapana na marefu suala la waamuzi kabla ya ligi kuanza ili kuhakikisha hawavurugi uhondo wa ligi.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4413