Sep 5, 2010, 12:20 pm TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-07-27 13:27:00
Kocha Profesa wa Serbia atua Simba
Huyu huenda akamrithi Patrick Phiri wa Simba kama mambo yatakwenda vizuri habari kamili soma pembeni
LAMPS COLLIN
SIMBA imemtumia mkataba wa miaka miwili kocha wake wa zamani, Cirkovic Milovan wa Serbia ambaye anajulikana kwa jina la Profesa.

Klabu hiyo ya Msimbazi jijini Dar es Salaam ipo dakika za mwisho kuuvunja mkataba na kocha wao wa sasa, Patrick Phiri ambaye amekuwa akipiga 'kiswa
ili kingi' kuhusu kurejea kwake.

Phiri alizungumza na Mwanaspoti tena jana Jumatatu na kusema: "Kama nilivyokwambia wiki iliyopita nina matatizo, bado sijafahamu siku ya kurudi, lakini ni siku yoyote nikimaliza matatizo."

Habari za ndani zinasema kuwa viongozi wa Simba walikuwa wamempa Phiri mpaka jana Jumatatu na iwapo asingerudi wangesitisha mkataba wake ambao umebakiza miezi mitatu.

Ndio maana wamemtumia mkataba Milovan ambaye amewahi kuifundisha Simba mwaka juzi, ambao aliupata juzi Jumapili na akikubali ataanza kazi Agosti Mosi ila akigoma atakuja Sam Timbe wa Uganda, ambaye ni chaguo la pili kwa sasa.

Kocha wa zamani wa Yanga, Sredojevic Milutun 'Micho' ambaye sasa yupo Al Hilal ya Sudan amewahi kumsifu Milovan kuwa ni bonge la kocha na kwao Serbia huitwa Profesa.

Sifa kubwa ya Milovan ni kuwa amewahi kuwa msaidizi wa kocha bora wa Serbia, Bora Milutinovic ambaye mwaka 1986 aliifikisha Mexico katika robo fainali ya Kombe la Dunia.

Milovan alikuwa msaidizi wa Bora Milutinovic walipokuwa wanainoa klabu ya FC Vojvodina Novi Sad ya Serbia ingawa walifungwa na Atletico Madrid katika Kombe la Uefa.

Kwa mara ya kwanza, Milovan alijiunga na Simba Februari 20, 2008 akichukua nafasi ya Mbrazili, Nielsen Elias ambaye alikuwa ameingia mitini baada ya kukaa kwa siku 36 tu.

Milovan aliondoka katika mazingira ya kutatanisha, baada ya ligi huku Simba wakisema kuwa angerejea Juni 15, mwaka 2008 lakini haikuwa hivyo mpaka sasa.

Kocha huyo aliyekuwa analipwa dola 2500, alitaka aongezewe mshahara baada ya kocha wa Yanga wakati huo, Dusan Kondic kumshauri afanye hivyo kwani yeye alikuwa analipwa dola 10,000.

Alipotua Tanzania mwaka 2008, mechi yake ya kwanza kuiona ilikuwa ni sare ya 1-1 kati ya Simba na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru.

Safari hii akija Milovan hawezi kuwaona wachezaji ambao alikuwa akiwapenda sana; Ulimboka Mwakingwe, Moses Odhiambo na Julius Mrope.

Milovan aliipa adhabu kali Prisons ya Mbeya alipoiongoza Simba kuifunga mabao 4-0 katika mchezo ambao ulichezwa kuanzia saa 7:00 mchana na kuonyeshwa moja kwa moja na kituo cha televisheni ya kulipia ya GTV.

Ni makocha wengi walipita baadaye akiwamo Krasimir Bezinski wa Bulgaria ambaye alitimuliwa kutokana na Simba kuboronga.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4412