Sep 5, 2010, 12:37 pm TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-07-27 13:12:00
Henry Joseph chupuchupu
OLIVER ALBERT
MAME Niang alichomoa bao dakika ya 87 na kuiepusha Kongsvinger na kipigo cha nne mfululizo kutoka kwa Tromso katika mchezo wa Ligi Kuu Norway uliochezwa juzi Jumapili.

Timu hiyo ambayo anaichezea kiungo wa Taifa Stars, Henry Joseph Shindika imekuwa haifanyi vizuri tangu kuanza kwa ligi hiyo na mashabiki wameitabiria kushuka daraja.

Tromso ndio walikuwa wa kwanza kupachika bao dakika ya 27 lililozamishwa na Bobbie Fribergda na kipindi cha pili baadae Henry ambaye anacheza kama beki wa kati katika timu hiyo alitolewa baada ya kushindwa kuonyesha kiwango kutokana na maumivu ya enka.

"Tutakaa sawa tu ingawa hali ni mbaya kwetu lakini nafikiri tunahitaji kuongeza nguvu katika kikosi chetu ili tuweze kufanya vizuri," alisema Henry.

"Ukiangalia timu yetu, wachezaji wengi wana umri mkubwa na kocha ameliona hilo na hapa tunachoomba tubaki kwenye ligi ili kocha asajili yosso," alijipa moyo Joseph, ambaye alikwenda Norway akitokea Simba.

Kongsvinger inashika nafasi ya 15 kati ya timu 16 zinazoshiriki ligi hiyo ikiwa na pointi 12 baada ya kucheza mechi 18, imefungwa 12, imeshinda tatu na imetoka sare mara tatu.
Rosenborg ndio inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 40 baada ya kushinda mechi 11 na kutoa sare saba.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4405