Sep 5, 2010, 11:59 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-07-24 12:23:00
Saa mbili za jasho na damu Yanga
MICHAEL MOMBURI
HIVI ndivyo kikosi cha Yanga kilivyofanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam jana Ijumaa.

Saa 3.25 asubuhi: Wachezaji wa Yanga wamekusanyika katikati ya uwanja kuomba dua, dakika mbili baadaye wanaanza mchakamchaka wakati kocha wa Azam, Itamar Amorin amekaa kwenye benchi la upande wa Simba akiwatazama.

Saa 3.30: Wanaingia wauguzi wawili wazungu wa zahanati ya Trauma yenye mkataba na Yanga na kocha Kosta Papic anatoka pembeni ya uwanja na kuwagombeza wazungu hao huku mtunza vifaa, Mpogolo akipanga koni za mazoezi.

Saa 3.33: Wachezaji wamejipanga makundi kuchezea mipira huku Papic akiwafuata makipa na kumwambia kitu Yaw Berko. Wanafunzi wa Shule ya Msingi Maalumu ya Mtoni, ambayo inahusisha watoto wenye mtindio wa akili wanakimbia riadha kuzunguka uwanja wakiwa wamevaa jezi za njano.

Saa 3.46: Papic anachekelea adhabu ya Nsa Job na Kenneth Asamoah ya kupiga 'push-up' waliyopewa na kundi lao baada ya kukosa mipira.

Saa 3.50: Papic na mwanaye,Todor wako katikati ya uwanja wakiangalia makundi ya wachezaji nane nane yalivyokuwa yakichezea mipira ingawa walikuwa wakimteta kwa kunong'onezana kiungo Mghana Ernest Boakye.

Saa 3.58: Zoezi la kuchezea mipira linamalizika, Papic anawapanga wachezaji kwenye makundi mawili.

Saa 4.00: Kila linaanza kukimbia kwa kuzunguka uwanja, kila baada ya raundi kila kundi linasimama kuvuta pumzi kwa dakika mbili na kuendelea kukimbia tena.


Saa 4.12: Wanakwenda kunywa maji, wakiwa wanaondoka kurudi kucheza mechi Jerry Tegete anaulizwa na shabiki mbona kwanini amepunguza `Mzuzu', naye anamjibu kuwa ulikuwa unamtisha sana Mpangala.

Saa 4.18: Papic anapanga magoli matatu; moja katikati ya uwanja anamwambia Nelson Kimathi akae goli la katikati, Ivan Knezevic anapangwa Kaskazini na Berko goli la Kusini. Mechi inaanza wachezaji wakijipanga kwa jinsi mpira unavyokwenda.

Saa 4.23: Mashabiki wanaguna baada ya Nurdin Bakari kukosa goli la wazi akiwa na Berko.

Saa 4.25: Beki Hood Mayanja anampiga chenga ya mwaka Nadir Cannavaro na kuzidi kuteka akili za mashabiki wa Yanga. Nsa Job anamfunga Ivan.

Saa 4.35: Yahya Tumbo anamfunga Kimathi, mtoto mwenye miaka sita anayesumbuliwa na mtindio wa ubongo anaingia uwanjani Mbaga anamtoa.

Saa 4.38: Mbaga anamfunga Ivan, Kimathi anaokoa shuti la Abdi Kassim.

Saa 4.40:Tegete anatoka uwanjani anavua njumu ya kushoto na kuvaa raba ya kawaida na kurudi ndani bila Papic kujua.

Saa 4.47: Makipa Yaw na Ivan wanabadilishana upande mpira unaendelea, Tegete anamfunga Berko huku Chuji akitaniana na Cannavaro " We Mpemba wewe..Chuji Dodoma..piga huku." Nsa anamfunga tena Ivan.

Saa 4.53:Papic anampigia kelele Tegete achangamke, Chuji anapiga shuti la mita 40 Berko anapangua anashangiliwa.

Saa 4.56: Tegete anamfunga Kimathi, Papic anakataa kwa madai kuwa mpira uligonga koni ambayo ilikuwa kama mlingoti wa goli. Wanabishana dakika kadhaa. Mbaga anakung'uta shuti anamfunga tena Ivan.

Saa 5.00: Papic anawaambia wachezaji wachangamke kwani zimebaki dakika saba mazoezi yaishe. Tegete anaangushwa eneo la hatari na Bakari Mbegu. Tegete anapiga penalti Berko anapangua na kushangiliwa.

Saa 5.07: Papic anapuliza kipenga kumaliza mazoezi, wanakusanyika kati wanafanya zoezi la kunyanyua mikono juu, chini na kuchezesha viungo safari hii kipa Berko ndio anaongoza Papic kasimama nyuma yake.

Saa 5.10: Wanamaliza kwa sala, Papic yupo katikati ya duara la wachezaji akiwasisitiza jambo halafu wanatawanyika kuchukua vifaa na kwenda kupanda basi kuelekea kambini Jangwani.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4397