Sep 5, 2010, 12:18 pm TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-07-20 11:13:00
Vuvuzela zawapokea Nchunga, Mosha
Kanakamfumu wale wachezaji watatu wa Yanga hamna kitu kabisa,ni kama Jama Mba tu, yaani kama yule Asamoh ni kama Obina wa Simba tu, sijui wamemsajili wa nini. Mh! mimi hata siingilii, ila hilo nalo neno, bora wangemrudisha Mwaikimba tu we unafikiri watamzidi Chuji kweli wale!.
Clara Alphonce

TARUMBETA maarufu za vuvuzela ndizo zilizotumika kuwapokea viongozi wapya wa klabu ya Yanga baada ya Kamati ya Uchaguzi ya klabu hiyo kuwatangaza rasmi jana.

Kamati hiyo chini ya makamu mwenyekiti wake, Ridhiwani Kikwete ilimtangaza wakili Llyod Nchunga kuwa mwenyekiti mpya wa klabu hiyo ya Mtaa wa Twiga na Jangwani huku makamu wake akichaguliwa Davis Mosha.

Matokeo hayo yalitangazwa jana saa 2.00 asubuhi baada ya saa zaidi ya 12 za mvutano na zoezi gumu la kuhesabu kura lililoendelea usiku kucha kwenye ukumbi wa PTA, viwanja vya maonyesho vya Mwl Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao walipigiwa kura juzi Jumapili na wanachama zaidi ya 3,000 wa klabu hiyo ambao waliwapa jukumu la kuiongoza klabu hiyo kongwe kwa kipindi cha miaka minne.

Baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo ambayo mwenyekiti (Nchunga) hakuwapo ukumbini, makamu wake (Mosha) aliwashukuru wanachama wa klabu hiyo kwa jukumu zito ambalo wamewakabidhi.

Baadhi ya wanachama wa klabu hiyo waliyapokea matokeo hayo kwa kushangilia kwa kupuliza zumari maarufu zilizotumika kwenye fainali za Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini, vuvuzela.

Mosha kwa upande mwingine, aliahidi kushirikiana na wenzake ili kuzika tofauti na makundi ambayo yamekuwa yakijitokeza katika klabu hiyo.

Pia, (Mosha) alisema kuwa uongozi wa klabu hiyo hautasita kuwajumuisha kwenye kamati ya utendaji baadhi ya wagombea walioshindwa na wanachama wengine maarufu wa klabu hiyo ili kujenga klabu imara na inayojiendesha kwa mafanikio.

Katika uchaguzi huo, Nchunga alifanikiwa kuibuka mshindi baada ya saa 13 za zoezi gumu lililoanza saa 2.00 usiku na kuendelea hadi 2.00 asubuhi jana baada ya kupata 1,435 akifuatiwa na Francis Kifukwe (370) na Mbaraka Igangula (305), Abeid Abeid ' Falcon' (301) na Edgar Chibura (65).

Naye Mosha ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa klabu ya soka ya Moro United iliyoshuka daraja msimu huu alipata kura 2,142 akimshinda Constantine Maligo aliyeambulia kura 55.

Ridhiwani Kikwete ambaye alikesha ukumbini hapo na kamati yake aliwataja wajumbe wanane wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo kuwa na kura zao katika mabano kuwa ni Mzee Yusuph (1,317), Mohammed Bhinda (1,458), Sarah Ramadhan (1,500), Salim Rupia (1,231), Tito Ossoro (1,460), Charles Mugondo (1,300), Ally Mayay (1,734) na Theonest Rutashoborwa, kura 1,225.

Baada ya Ridhiwani kuwatangaza viongozi wapya alimkaribisha mjumbe wa baraza la udhamini wa klabu hiyo ambaye pia ni mfadhili Yussuf Manji ambaye alirejea ukumbini hapo nusu saa kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo ili kutoa maneno machache kwa uongozi mpya.

Katika nasaha zake, Manji ambaye alisema ni mdhamini ambaye si mpigakura wa klabu hiyo alikuwa ukumbini hapo baada ya kuondoka juzi na kuwapongeza viongozi hao wapya kwa kuchaguliwa kuingia madarakani na kuahidi kufanya nao kazi bega kwa bega kwa maslahi ya klabu hiyo.

Hata hivyo, upigaji wa kura katika uchaguzi huo haukuwa na utaratibu nzuri kiasi cha kudaiwa na wengine kuwa uliwanyima haki yao ya kupiga kura.

Baadhi yao walitishia kuondoka katika uchaguzi kwa madai kuwa makamu mwenyekiti huyo (Ridhiwani) alikuwa ameharibu uchaguzi huo.

Awali, uchaguzi huo uliingia dosari baada ya mgombea nafasi ya uenyekiti, Kifukwe (Francis) kupanda jukwaani na kutangaza kujiondoa katika uchaguzi huo kwa madai ya kuwapo watu waliokuwa wakiendelea kufanya kampeni siku ya uchaguzi.

Kitendo hicho kilisababisha uchaguzi huo kusimama kwa muda baada ya wafuasi wake (Kifukwe) kutaka kuzusha vurugu kwa madai kuwa mgombea wao alikuwa amehujumiwa.

Aliyekuwa mgeni rasmi kwenye uchaguzi huo, Naibu Waziri wa Habari , Utamaduni na Michezo, Joel Bendera alitumia busara zake na kusema kuwa hawatambui kujiondoa kwa mgombea huyo (Kifukwe) kwani ni kinyume na taratibu.

Badala yake aliwataka watu waendelee na uchaguzi na wale wanaotaka kumpigia kura Kifukwe waendele kufanya hivyo.

Wakati wa wanachama hao kupiga kura kulikuwa na hali ya utulivu wa hali ya juu huku wanachama hao wakiwa wamekaa makundi makundi huku wakijadili ni nani atakuwa kiongozi wao mpya huku wengine waliomaliza kupiga kura waliondoka bila kusubiri matokeo.

Nje ya ukumbi huo tangu juzi hadi jana, askari polisi wenye sare pamoja na makachero walionekana wakisimamia uchaguzi huo na kulazimika kukesha wakisimamia mchakato huo wa kuwapata viongozi wapya wa klabu hiyo kongwe nchini.

Uchaguzi huo umekamilisha muhula wa uongozi wa Imani Madega ambaye ameiongoza klabu hiyo ambayo msimu ujao itaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) baada ya kumaliza katika nafasi ya pili.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4380