LONDON, ENGLAND
THIERRY Henry amemtaka Cesc Fabregas asithubutu kuhamia Barcelona na badala yake aendelee kukaa Arsenal. Nyota huyo ambaye alikuwa akipachika mabao mara kwa mara Arsenal alinyakuliwa na Barcelona, Juni 2007 baada ya kuitumikia Arsenal kwa miaka nane.
Na akiwa Barcelona, alishindwa kuwika kabla ya kuhamia Marekani msimu huu.
Henry mwenye miaka 32, amesema ingawa ameondoka Arsenal, bado ni shabiki wa timu hiyo.
Klabu hiyo ya Hispania imeweka wazi kwamba inataka kumnyakua mchezaji huyo mwenye miaka 23 lakini Arsenal ilikataa ofa yao ya pauni milioni 30 iliyotangazwa awali.
Henry alisema: "Ni kazi ngumu kumnasa mchezaji huyo kwa sababu ingawa anatoka Barcelona lakini anaipenda Arsenal.
Henry anasubiri changamoto mpya baada ya kuhamia katika kikosi cha New York Red Bulls wiki iliyopita. Nyota huyo anategemea kumaliza soka lake katika klabu hiyo.
Lakini kitu cha kichekesha ni kwamba mechi ya kwanza ya Henry katika timu mpya itakuwa dhidi ya wapinzani wa Arsenal, Tottenham, Ahamisi wiki hii.