Sep 5, 2010, 12:38 pm TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-07-17 12:15:00
Rooney alipwa bilioni 70
LONDON, ENGLAND
MSHAMBULIAJI wa Manchester United, Wayne Rooney atasaini mkataba wa mpya katika klabu yake wenye thamani ya pauni milioni 35 (sawa na shilingi bilioni 70 za Tanzania). Mkataba huo utamfanya nyota huyo akae Manchester United mpaka mwaka 2015.

Rooney atakuwa nyota anayelipwa zaidi Manchester United ambapo atakuwa akipata pauni 130,000 kwa wiki. Na imeelezwa kuwa mchezaji huyo atasaini mkataba huo kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu England.

Mkurugenzi wa Manchester United, David Gill atakaa na Rooney na wawakilishi wake baada ya mchezaji huyo kutoka Barbados, ambapo amekwenda kwa ajili ya mapumziko.

Ingawa Rooney hana mpango wa kuondoka Manchester United, viongozi wa Old Trafford, wanataka nyota huyo aongeze mkataba wa muda mrefu, ambao utasaidia kuziweka mbali klabu nyingine zinazomtamani.

Mazungumzo ya mkataba mpya kwa mchezaji huyo yalichelewa kutokana na kusubiri kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia.
Rooney, amekuwa akilipwa pauni 90,000 kwa wiki nyuma Rio Ferdinand anayelipwa pauni 120,000 kwa wiki.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4362