Sep 5, 2010, 12:33 pm TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-06-17 11:29:00
Eriksson:Kongamano lije tujadili Jabulani
SVEN-Goran Eriksson ametaka kuitishwa kwa kongamano la wanasoka na makocha kujadili mpira wenye utata wa Kombe la Dunia na kushauri Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) isikilize maoni yao.

Kocha huyo wa Ivory Coast anadai kuwa mpira huo unaojulikana kwa jina la Jabulani unawaweka makipa kwenye hali ngumu wakati wa fainali za Kombe la Dunia zinazoendelea nchini Afrika Kusini.

Mpira huo uliotengenzwa na kampuni ya Adidas umekuwa ukilaumiwa sana, huku kipa wa England, David James akiuelezea kuwa ni wa kutiosha na Gianluigi Buffon na Mark Schwarzer, makipa namba moja wa Italia na Australia, wakiuelezea kuwa "hautabiriki".

"Naelewa kuwa makipa hawaufurahii, na nadhani mamlaka husika lazima ziwasikilize," alisema Eriksson. "Nadhani suala hilo halina budi kujadiliwa. Wachezaji, makocha na hata makipa hawana budi kukusanyika kujadili. Watu hawana budi kuwasikiliza hasa maoni ya makipa, kwa sababu mpira hauwatendei haki."

Kipa wa England, Robert Green aliruhusu bao la kufedhehesha alipopangwa kikosi cha kwanza na kumuweka benchi James katika mechi dhidi ya Marekani, ingawa alikanusha kuwa mpira ndio uliosababisha bao hilo.

Pia alikanusha madai kuwa aliathiriwa na uamuzi wa Fabio Capello kutangaza kikosi saa mbili kabla mchezo kuanza, sera ambayo kocha huyo wa England amepanga kuendelea nayo kesho wakati nchi hiyo itakapovaana na Algeria.

England ilikuwa inafundishwa na Eriksson kwenye fainali zilizopita za Kombe la Dunia na kocha huyo Mswidi amesema baada ya sare ya bila kufungana na Ureno juzi, Ivory Coast ni timu nzuri kufanya nayo kazi.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4229