Sep 5, 2010, 11:56 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-06-17 11:27:00
Komandoo ashikiliwa Sauzi
SI Tanzania tu ambako kuna makomandoo wanaouuza tiketi za magendo za kuingilia uwanjani, hata Sauzi wapo.

Polisi jijini hapa wanamshikilia kijana mmoja kwa kuuza tiketi za kuingilia katika mechi ya Brazil na Korea Kaskazini kwenye Uwanja wa Ellis Park juzi Jumanne.

Brigedia Sally de Beer alisema jana kuwa kijana huyo alikamatwa juzi Jumanne jioni akiuza tiketi za mechi hiyo nje ya Uwanja wa Ellis Park.

Alisema bado wanaendelea kumshikilia kijana huyo huku wakifanya uchunguzi zaidi wa matukio ya uuzwaji wa tiketi ambazo zimetapakaa katika viwanja mbalimbali.

Mechi ya Brazil na Korea Kaskazini ilikuwa ni miongoni mwa mechi ya kuvutia, licha ya kuwa mashabiki walikuwa katika wakati mgumu
kutokana na baridi kali jijini hapa.Mamlaka ya hali ya hewa ilitoa taarifa kuwa hali ya hewa
ilikuwa 2C.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4228