Sep 5, 2010, 12:39 pm TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-06-17 11:24:00
Baridi yakimbiza mashabiki uwanjani
Drodba na Ronaldo baada ya mchezo wao kumalizika Ureno na Ivory Cost zilitoka 0-0
MAMBO manne yalijitokeza juzi Jumanne
usiku wakati Brazil ilipoifunga Korea
Kaskazini mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Ellis
Park jijini hapa, lakini mashabiki wakaukimbia
uwanja baada ya dakika 75.

Ukiondoa kukatika kwa umeme kwa takribani
dakika moja,wakati timu hizo zikipasha, tukio
kubwa ilikuwa ni kuona timu hizo zikicheza
mchezo huo wa Kundi G bila kuwepo kwa
faulo yoyote kwa dakika 13 za mwanzo.

Timu hizo zilionyesha kandanda safi huku
Korea Kaskazini ikijihami na wachezaji sita,
huku kukiwa hakuna faulo yoyote mpaka
dakika ya 13 na katika mechi yote kukiwa na
faulo tisa tu.

Kutokana na timu zote kucheza mchezo wa
nafasi na kutaka kujiachia ndio maana mchezo
ulikuwa na kadi moja tu ya njano aliyopewa
Remires dakika ya 88, ikiwa ni muda mchache
tangu aingie akitokea benchi.

Jambo jingine katika mechi hiyo ni zaidi ya
robo ya mashabiki wote 54, 331 waliohudhuria
mechi hiyo kuondoka uwanjani dakika ya 75
kutokana na baridi kali jijini hapa.

Brazil ilipata bao la kwanza dakika ya 55
lililofungwa kiufundi mkubwa na Maicon kabla
ya Elano kufunga kutoka upande huo huo wa
wingi ya kulia dakika ya 72 huku Korea
Kaskazini wakifunga bao lao moja dakika ya 89
kupitia kwa Ji Yun Nam.

Mashabiki waliojitokeza uwanjani hapo
walijikuta katika wakati mgumu kutokana na
hali ya hewa kusomeka kuwa ilikuwa katika
nyuzi 2C, jambo ambalo lilifanya baadhi ya
maeneo ya Johannesburg kujaa barafu.

Jambo jingine katika mchezo huo ni kuona
Korea Kaskazini ikijihami kwa kutumia
wachezaji sita na hata iliposhambulia mabeki
wanne waliendelea kubaki nyuma bila kwenda
mbele.

Hata hivyo kuzubaa kwa beki wao wa kushoto
Ri Jun II kuliiponza timu hiyo na kujikuta
ikifungwa mabao 2-1.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4227