Sep 5, 2010, 11:44 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-06-17 11:23:00
Mgambo wagomea Kombe la Dunia
JESHI la Polisi limeongeza ulinzi katika
viwanja vinne ambako kunafanyika mechi za
Kombe la Dunia kutokana na walinzi
waliokuwa wamewekwa kwa kazi hiyo
kugoma.

Licha ya polisi kuwemo katika ulinzi wa
viwanja hivyo, kulikuwa pia na watu maalumu
waliokuwa wameajiriwa kwa ajili ya kusaidia
ulinzi katika viwanja vyote kumi vinavyotumika
kwa fainali za Kombe la Dunia.

Zaidi ya walinzi 1,000 walikuwa wameajiriwa
kwa ajili ya kulinda viwanjani wakati wa
Kombe la Dunia kwa kusaidiana na Jeshi la
Polisi.

Lakini walinzi hao wamegoma kuendelea na
kazi hiyo na kufanya mechi ya Brazil na Korea
Kaskazini juzi Jumanne usiku kulindwa na
Polisi tu.

"Mkutano uliofanywa kati ya Idara ya Usalama
na Kamati ya Maandalizi, tumeamua kuweka
utaratibu mpya, sasa viwanja vinne vya Port
Elizabeth, Cape Town, Soccer City na Ellis
Park vitalindwa na polisi tu," alisema Meja
Jenerali Nonkululeko Mbatha.

Zaidi ya walinzi 700 waligoma juzi Jumanne
saa tatu kabla ya kuanza kwa mechi ya Brazil
na Korea Kaskazini kwenye Uwanja wa Ellis
Park kwa madai ya malipo.

Walinzi hao walikuwa wamesimama nje ya
jengo wanalotolea vitambulisho maalumu (Fifa
Accreditation Centre)ambako walitarajiwa
kulipa fedha zao Randi 190 kwa kila usiku na
kwamba mikataba yao itasitishwa.

Kilichosababisha wagome ni kutokana na
mikataba yao kutoonyesha malipo
watakayolipwa baada ya kumalizika kwa
fainali za Kombe la Dunia.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4226