LAGOS, NIGERIA
BUKKY, ambaye amejizolea umaarufu kutokana na kuigiza pia ufanisi katika uandaaji filamu (prodyuza) ameingia katika kashfa nzito baada ya kubainika kuwa anapenda mapenzi ya jinsia moja.
Dada huyo amekuwa na kashfa ya kuiba wanaume za watu na kulala na wanaume mbalimbali sambamba na ugomvi.
Hayo ni baadhi ya mambo ambayo amekuwa akiyafanya katika miaka ya nyuma, lakini sasa ameibuliwa kashfa mpya ya mapenzi ya jinsia moja.
Na kibaya zaidi ni kwamba mwanamke huyo amekuwa akiiba wake za watu na mpaka habari hii inakufikia ameshakuwa na uhusiano na wanawake kadhaa.
Lakini hivi karibuni alijaribu kutafuta wanawake wengine walioolewa na kugonga ukuta kabla ya siri yake kuvuja.
Na imefahamika kwamba mwanamke huyo amekuwa na akionywa na wanaume mbalimbali kutojaribu kusogelea wake zao.