Sep 5, 2010, 11:49 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-06-08 09:50:00
Emeka Ike bafuni na Muma Gee
LAGOS, NIGERIA
MWANAMUZIKI Muma Gee wa Nigeria ameibuka na 'kuruka kimanga' kwamba hana uhusiano wa kimapenzi na muigizaji wa Nollywood, Emeke Ike na kwamba hafikirii kama kuna siku atamtamani mwanaume huyo.

Hata hivyo Muma Gee alionekana kuwa karibu na muigizaji huyo katika mashindano ya Nyota wa Nigeria yaliyoitwa Gulder Ultimate Search, ambayo yalimalizika hivi karibuni na kuhusu hilo Muma Gee alisema:

"Nilikuwa karibu na Emeke kwa kuwa niliona ni mtu mwenye busara katika kundi hilo. Niliona kwamba ni mtu ambaye angalau alikuwa na hadhi yangu.

"Nilifahamiana na Emeka Ike kabla ya mashindano hayo kwa hiyo sikuona sababu ya kuwa mbali naye. Nilikaa katika mashindano kwa siku kadhaa, familia yangu haikuwepo, ilibidi kuwa na mtu wa kuzungumza naye.

Lakini cha kushangaza ni kwamba watu walianza maneno kwamba nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwanaume huyo jambo ambalo si ukweli.
"Watu wanatakiwa kuwa na upeo wa kutofautisha urafiki wa kawaida na mapenzi."

Na kuhusu habari kwamba waliwahi kufanya mapenzi bafuni dada huyo alisema: "Siwezi kufanya jambo kama hilo kwa kuwa najiheshimu mwenyewe vilevile namheshimu Emeke na mke wake.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4181