LAGOS, NIGERIA
MOSUNMOLA Filani ni mmoja wa wadau wakubwa wa filamu nchini Nigeria kutokana na juhudi zake katika uandaaji na uigizaji wa filamu, lakini tatizo la dada huyo ni moja tu, wizi wa wanaume za watu.
Na safari hii dada huyo amekuwa na uhusiano na Muyiwa Ademola, ambaye ni mwanaume aliyeoa. Lakini amekwaa kisiki kwa kuwa mke wa Muyiwa amekujaa juu na kumwambia dada huyo achague moja; amuache mwanaume huyo au apotezwe mjini.
Mke wa Muyiwa ametuma ujumbe kwamba ameandaa adhabu kali kwa muigizaji huyo na iwapo adhabu hiyo ikimshukia ni wazi kwamba atahama mjini.
Dada huyo amesema kwamba ameandaa tindikali kwa ajili ya kumjeruhi Mosunmola na kumfanyia mambo mengine ya kihuni kama ataendelea kutembea na mume wake.
Na imefahamika kwamba ujumbe huo umekuwa sumu kali kwa Mosunmola ambaye sasa ameanza kumuogopa Muyiwi kama ukoma.