WENGI wanaingia kwenye uhusiano wakitaka raha…raha katika suala zima la mahaba, raha katika uchumi na mambo mengine kadhaa wa kadhaa.
Baadhi ya watu hasa wanawake, wanaamini kwamba kuingia kwenye ndoa maana yake ni kupata maisha bora…kwamba kama alikuwa hajawahi kuvaa mikifu ya dhahabu basi sasa kwa sababu anaolewa, ataipata, kama alikuwa ana aina fulani ambayo huenda hayakuwa mazuri sana, anajipa imani kwamba aaah sasa kila kitu ni poa.
Ni imani hii ndiyo inayosababisha baadhi ya ndoa kuanguka haraka…ni kwamba baadhi ya watu wanakuwa na matarajio makubwa mno wanapoingia kwenye ndoa.
Anapoona mambo yanakwenda kombo kwa maaana ya kuwa tofauti na matarajio yake, wengine wamekuwa wakikata tamaa na kuanza kujiuliza aaah yanini sasa kuwa kwenye ndoa hii, mbona yale niliyokuwa nikitegemea siyaoni.
Kuna wengine pia kwa mfano huenda wako tayari kwenda anafikiri kwamba maana ya kuwa kwenye ndoa au kuwa kwenye uhusiano ni kuwa kila kitu awe anapata nanilihii….mwenzi wake akimwambia nimechoka inakuwa ni balaa.
Wapo wanawake wamekimbia ndoa kwa sababu tu mwanaume anapenda mno…eeeh utaona wengine ni kama dozi ya dawa, asubuhi anataka, mchana anataka, usiku ndio usiseme, kiasi kwamba wanawake wengine wanaona kama ni adhabu.
Au kuna wengine kila siku anataka, ukimnyima nyumbani hapakaliki. Kitaalam kuwa hivi si sahihi hata kidogo. Ni vizuri kuangalia vitu vingine vinavyowafanya mpendane sio nanihii tu, kwani pia kiafya sio nzuri sana…yaani kushiriki kila siku.
Maisha bora katika ndoa yanamuhitaki kila mmoja kumfikiria mwingine na kumfanyia yale ambayo ni mazuri, yale ambayo hata yeye akifanyiwa atajisikia raha.
Je, wewe unayesoma makala haya unamfanyia yaliyo mazuri mwenzi wako? Ni swali ambalo kila mmoja wetu anapaswa kulitafakari na kuchukua hatua. Ukweli ni kwamba uzuri wa ndoa au uhusiano kwa ujumla ni kwa kila mmoja kupata muda wa kutafakari namna ya kupeana raha.
Kutegemea raha tu kutoka kwa mwenzi wako ni jambo zuri, lakini kwanza kabla ya kusubiri kupewa hiyo raha, jitahidi wewe ndio mtoaji wa raha. Wanaume kwa mfano, baadhi yao wamekuwa wakilalamikiwa kujipa raha zaidi wao…utakuta jamaa yaani yeye mwanamke akimwambia mhhh bado, haelewi, wengine utaona hata wanawatolea kauli chafu..aaah bwana eeeh mimi nimechoka bwana.
Si kweli ni kwamba mwanaume unapaswa kumtosheleza mwenzi wako, ndipo ufuatia wewe. Kitaalam ni kwamba ni kweli kuwa mwanaume ni mwepesi zaidi kusisimka…inakadiriwa ni wastani wa dakika tatu wakati kwa wanawake ni dakika 11, kwa maana hiyo ninachotaka kusema ni kwamba mwanaume anapaswa kuwa mbunifu zaidi wa kuangalia ni namna gani anaweza kufanya ili kumfanya mwenzi wako naye awe mwenye kuridhika.
Kiafya na hata katika misingi ya dini si vizuri mwanaume kumuacha mwanamke katika hali ya kutotosheka kwa namna yoyote iwe ni kimahaba au nyingine yoyote unayoijua. Mwanaume anapaswa kufanya awezalo kumfanya mkewe awe ni mwenye kumpenda zaidi.
Eeeh kama ni katika mahaba wakati mwingine mwanaume unapaswa kujua ni namna gani mwanamke anakuwa kweli ameridhishwa au hajarishwa. Kwa mfano kitaalam dalili za kujua mwanamke ameridhishwa nawe ni kutokuwa mwepesi wa kutoka sehemu ambayo mlikuwa mmepumzika, wengine hupatwa usingizi nk.
Lakini hata kama labda mwenzi wako anaonekana kutokupa raha, jitahidi kuendelea kufanya kila linalowezekana kutenda raha, hatimaye naye anaweza kuwa mwenye kutenda raha.
Kwa ujumla watu wanapenda raha….hata kama labda unafikiri mwenzi wako si mwaminifu, unachopaswa kufanya ni kuangalia wapi kuna kasoro, huenda mmhh humpi raha…kuna wengi wamekuwa wakisema aaah nampa raha sana, lakini jitu lenyewe ndio vile tena…hayo umesema wewe…ukitaka kupata ukweli muulize mwenyewe kama kweli anapata anachokitaka.
Sababu mojawapo ya wanawake wengi kukimbiwa kwenye ndoa ni kauli za nyodo….aaah bwana eeeh haya mambo yako haya mie siyawezi…uwiii…unataka kuniua mie…haya mambo ya vijana haya…haya mastaili yako kawafanyie makahaba, mimi siwezi”….nk.
Pia wapo wanaume wenye kauli chafu za kunuka…kauli mbovu ndizo zimekuwa msingi wa nyumba nyingi kuvunjika, watu wanaona eeeh naona hapa ni mvua tu inanyesha, itabidi nitafute japo kitanda kidogo nijihifadhi na mvua ya matusi, mvua ya kudharauliwa nk…matokeo yake kwa bahati mbaya wengine wanajikuta wanahamia huko moja wa moja. Hii ni kwa pande zote.
Je una maoni wasiliana na mtaalam wa uhusiano aliyesajiliwa na serikali (Social Welfare Counselor), Dismas Lyassa kwa simu 0712183282, email:globalsourcewatch@gmail.com