Sep 5, 2010, 11:52 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-05-29 12:19:00
Lampard, Christine katika wakati mgumu
Frank Lampard
LONDON, ENGLAND
HUKU kikosi cha England kikijiandaa kutua Afrika Kusini kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia, Frank Lampard anaonekana kuwa na wakati mgumu kukubaliana na ukweli kuwa atalazimika kuwa mbali na mpenzi wake Christine Bleakley kwa wiki kadhaa.

Na Lampard anafahamu 'mkwara' wa kocha wa England, Fabio Capello ambaye amebainisha kwamba hataki kuona wapenzi, wala wake wa wachezaji katika kambi yake nchini Afrika Kusini.
Katikati ya wiki hii Lampard na dada huyo walikuwa wakionekana pamoja mara kwa mara jambo ambalo limetafsiriwa kwamba walikuwa wanaagana.

Lakini ingawa kocha wa England amesema wachezaji wake hawataruhusiwa kuonana na wapenzi wao katika kipindi chote cha mashindano, wanawake hao wamesaka hoteli za karibu na watahudhuria mechi mbalimbali. England inatarajia kukwaana na Japan, kesho Jumapili huko Austria katika mechi ya maandalizi.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4136