Sep 5, 2010, 11:49 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-05-29 12:17:00
Mtoto wa Beckham aanza mitindo
LOS ANGELES, MAREKANI
MTOTO wa nyoka ni nyoka. Brooklyn Beckham ambaye ni mtoto wa mwanamitindo Victoria Beckham na mwanasoka David Beckham sasa ameanza kutamani mitindo.

Mtoto huyo mwenye miaka 11 ameanza kutamani kuvaa kama baba yake wakati anapotoka. Mara kadhaa David Beckham amekuwa akivaa mavazi yanayobuniwa na mke wake na mtoto wao ameanza kutamani kuvaa kama David.

Brooklyn alivaa kama baba yake katika sherehe moja ya onyesho la mavazi jijini Los Angeles ambapo alikwenda na mama yake.

Katika sherehe hiyo Brooklyn alivaa suruali ya `jeans' nyeusi na shati la mikono mirefu huku akiwa amechomekea upande mmoja kama ambayo baba yake hufanya.
Na mtoto huyo pia alinyoa nywele kama baba yake.

Na jambo hilo huenda likamvutia zaidi Victoria 'Posh' ambaye amezama katika fani hiyo. Lakini wakati hayo yakiendelea Beckham alikuwa jijini London ambako alikwenda kwa ajili ya kuunga mkono timu yake ya Taifa iliyokuwa ikicheza na Mexico na kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4134