Venus atikisa kwa mavazi
MAVAZI ya Venus Williams katika michuano ya wazi ya Ufaransa ndio yamekuwa yakivutia watazamaji zaidi kuliko uchezaji wake.
Katika michuano hiyo inayoendelea, Venus amekuwa akivaa nguo zinazoonyesha mwili wake kwa kiasi kikubwa na mara nyingi waandishi wa habari wamekuwa wakimuuliza kuhusu nguo badala ya mbinu zake za ushindi.
Dada huyo amekuwa akivaa nguo zinazofanaa na mwili wake na hivyo kuonekana kama vile mtupu.
Msemaji wa michuano hiyo, Christophe Proust alisema: "Nguo zake zinafanana na mwili lakini hayupo uchi, sijapata malalamiko yoyote."