BAADA ya mafanikio ya timu hiyo kutwaa ubingwa wa England na Kombe la FA, nyota mbalimbali wa Chelsea wanajipanga kujiunga na timu zao za taifa kwa ajili ya fainali ya Kombe la Dunia.
Habari njema ni kuwa staa wa Chelsea na Ghana, Michael Essien anaendelea vizuri na anafanya mazoezi maalumu kwenye uwanja wa mazoezi wa Chelsea ulioko Cobham.
Essien ameiamba tovuti ya klabu yake kuwa anaendelea vizuri na hivi karibuni alikutana na viongozi wa Shirikisho la soka Ghana kuongelea maandalizi ya Kombe la Dunia.
Amesema kwa sasa hataki kujipa presha ya kujiunga na timu ya Ghana lakini anachotaka ni kupona vizuri.
Essien amedokeza watu wengi wa Ghana wamekuwa wakiwasiliana naye na kumwombea ili acheze kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Essien amesema ana matumaini ya kucheza fainali za Kombe la Dunia lakini bado anajisikilizia.
Amedai kitu muhinu ni kuwa fiti kwanza kutokana na kuwa hajacheza soka tangu Januari.