Sep 5, 2010, 11:57 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-05-22 14:04:00
Manchester United
KUNA maandalizi kamambe ya msimu ujao na Manchester United imejipanga kucheza mechi za kirafiki Marekani na Canada, kwa mujibu wa Ofisa Mkuu Mtendaji wa klabu hiyo, David Gill.

Akizungumza katika uzinduzi wa ziara hiyo jijini New York, Gill amesema wamepania kufanya vizuri msimu ujao na anaamini ziara hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa timu hiyo.

"Ziara hizi zinasaidia kusogeza klabu karibu na wapenzi wao," aliongeza Gill, ambaye timu yake imevuliwa ubingwa na Chelsea.
"Unajua ziara kama hizi zinaongeza mashabiki na pia ni nafasi kwa wadhamini wetu kujitangaza.

Gill amesema ziara hiyo itaiweka timu hiyo vizuri kwa ajili ya msimu ujao.

Alisema pia wanapenda kwenda Marekani kwa kuwa viwanja vya huko viko kwenye hali nzuri.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
Mafowadi 11 watibuana Mtibwa Sugar
Taswa wajadiliana na Mkurugenzi wa Michezo
Mafisango aguna, aipa tano Azam
Mwingereza aanza kazi Zanzibar
Simba yaipeleka Yanga Kirumba
Poulsen ampiga tafu Phiri Simba
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=4085