Sep 9, 2010, 9:35 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-03-08 18:31:00
Timu za ligi kuu ya Bara
Danny Wagaluka wa Azam
YANGA

Yanga tayari ina tiketi ya kucheza Kombe la Shirikisho mwakani. Lakini endapo maajabu ya soka yakitokea Tanzania, Simba ikapoteza mechi zake zote tatu ilizobakiza na Yanga ikashinda zake tatu itatwaa ubingwa kwa kufikisha pointi 54.
Imebakiza mechi dhidi ya Moro United Machi 17, Simba Aprili 11 na Prisons Aprili 27, ambayo ndiyo ya funga dimba.

SIMBA
KWA asilimia 99 Simba tayari ni bingwa inahitaji pointi mbili tu kutimiza pointi 56 na kukabidhiwa kombe lake rasmi. Imesalia na mechi tatu dhidi ya Azam Machi 16, Yanga Aprili 11 na ile ya mwisho ya Mtibwa Sugar Aprili 27.
Kama ikiifunga Azam, Jumapili na kutwaa ubingwa itakuwa imeweka rekodi ya aina yake ya kutwaa ubingwa bila kupoteza mchezo.

AZAM

AZAM imepita njia mbaya ikazidiwa kete na Yanga kwenye mbio za kuwania nafasi ya pili ya Ligi Kuu ya Bara ambapo ingeshiriki Kombe la Shirikisho mwakani.
Timu hiyo yenye pointi 31 ikishinda mechi zake tatu zilizobaki dhidi ya Simba, African Lyon na Manyema itafikisha pointi 40 ambazo Yanga imeshazipita kitambo. Azam inachosaka sasa ni heshima ya nafasi ya tatu tu. Haishuki.

MTIBWA
Mtibwa habari yake ni kama ya Azam kwa vile zote zina pointi 31 lakini kwa tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa. Timu hiyo ya Morogoro inachowania sasa ni nafasi ya tatu kushiriki michuano ya kombe la Tusker. Ina mechi dhidi ya Toto Africa, Kagera na Simba. Haishuki.

MAJIMAJI
Majimaji ina pointi 24 na imesaliwa mechi tatu dhidi ya African Lyon, Prisons na Moro United lakini ikishindwa kukusanya pointi zote uwezekano wa kushuka daraja bado upo kwani timu za chini yake zinaweza kuivuta shati.
Lakini nahodha Patrick Betwel ana uhakika wako salama kwa vile mechi mbili za mwisho watakuwa nyumbani.

JKT RUVU
Ilikubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Simba wikiendi iliyopita na kubakia kwenye pointi zake 23 ambazo kama ikiendelea kulegalega nafasi ya kushuka daraja ipo palepale.
Ina mechi tatu pia dhidi ya Manyema, Toto na African Lyon ambazo zinaweza kuinusuru kama ikiamua.

AFRICAN LYON
Lyon inahitaji angalau kushinda mechi mbili zijazo dhidi ya Majimaji na Azam kupata pointi 26 ambazo zinaweza kuinusuru kwenye janga la kushuka daraja ingawa ikishinda mechi zote itakuwa na uhakika zaidi.
Mechi ya mwisho itavaana na JKT Ruvu ambayo nayo bado hakijaeleweka.

KAGERA SUGAR
Gonjwa linaloiandama Lyon ndio lile lile la Kagera ambayo imekuwa ikitoa upinzani mkubwa kwenye ligi kuu ya Bara misimu kadhaa.
Kagera ina pointi 20 ambazo zimeiweka kwenye nafasi ya nane ya msimamo ambayo kuna uwezekano ikashuka daraja au ikaenda juu isiposhinda dhidi ya Prisons, Mtibwa na Toto Africa.

MANYEMA
Ina pointi 18 zinazoiweka nafasi ya nne toka mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu ambako bado haijaponea kushuka kwani inaweza kuporomoshwa muda wowote.
Kuna timu tatu inazocheza nazo ambazo zimeshikilia roho yake ambazo ni JKT Ruvu, Moro United na Azam.

PRISONS
Jinamizi limezidi kuiandama Prisons kwani haitaki kubanduka kwenye nafasi tatu za mwisho mkiani mwa ligi ikiwa na pointi 17 kibindoni.
Uwezekano wa kupona unaweza kuwepo kama ikishinda mechi zake tatu zilizosalia dhidi ya Kagera, Majimaji na Yanga lakini iwaombee njaa wapinzani wake wapoteze.

TOTO AFRICA
Inapumulia mashine kama ilivyo Moro United. Ingawa ilimfunga Prisons mabao 3-0 wikiendi iliyopita bado ina nafasi ya kushuka ni kubwa.
Inachotaka sasa ni kushinda mechi zake zote tatu na kufikisha pointi 25 lakini iombee timu zingine ziboronge. Mechi zake zilizosalia dhidi ya Mtibwa, JKT Ruvu na Kagera inacheza nyumbani kwake jijini Mwanza.

MORO UNITED
Kocha wa Moro United, Juma Mwambusi yuko kwenye wakati mgumu kwani timu yake huenda ikashuka daraja kama ilivyokuwa kwa Polisi Dodoma 'iliyomfia' mikononi msimu uliopita. Ina pointi 15.
Imebakiza mechi tatu dhidi Yanga, Manyema na Majimaji lakini hali yake ni tete kutokana mwenendo wake wa hivi karibuni na mashabiki wake wamekata tamaa.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3642