Sep 9, 2010, 9:29 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-03-08 18:15:00
Chove atakiwa kuwa jasiri
Mfadhili wa Yanga,Yusuf Manji akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wa klabu hiyo,Lawrence Mwalusako. Manji amekaa na kocha Kosta Papic na kumaliza tofauti zao na kocha huyo kutangaza kwamba kila kitu kimekuwa sawa.
DORIS MALIYAGA

KATIBU Mkuu wa Chama cha Makocha Tanzania (Tafca) Eugen Mwasamaki amemwambia kipa wa JKT Ruvu, Jackson Chove kuwa:"Wewe ni Tanzania One, lakini jiamini zaidi."

Chove, ambaye pia yupo kwenye kikosi cha timu ya taifa 'Taifa Stars', ameonyesha kiwango cha juu katika mechi zote alizodaka na alipingia kipindi cha pili na kupangua penalti ya
Mussa Hassan 'Mgosi' baada ya Shaaban Dihile kuumia lakini ndani ya dakika sita za nyongeza, aliruhusu mabao mawili na kufanya matokeo kuwa 3-1 kwenye mechi kati ya timu hizo mbili, Jumamosi iliyopita.

Akizungumza na Mwanaspoti jana Jumatatu, Mwasamaki alisema, kiujumla Chove anazo sifa zote za kuwa kipa bora lakini alionyesha upungufu kwenye dakika za nyongeza zilizoongezwa kwenye mechi ya Ligi Kuu na Simba.

Alisema:"Tunaye kipa ambaye ni mzuri na huenda atatusaidia baadaye, lakini ana tatizo moja tu la kubabaika."

"Nina uhakika mabao yale mawili yaliyowapa ushindi Simba alikuwa na uwezo wa kuyazuia, lakini hali hiyo ya kutojiamini ilimwaribia," alieleza Mwasamaki.

Kwa upande wake, Chove alieleza changamoto kwake ni kujifunza kutokana na makosa lakini akajitetea bao la tatu lililofungwa na Uhuru Selemani lilikuwa la kuotea.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3635