Sep 9, 2010, 9:19 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-03-08 17:25:00
Johari amkubali Irine Uwoya
Johari
MICHAEL MOMBURI

KWA Johari, msanii mkali zaidi wa kike nchini ni Irene Uwoya lakini anawashangaa mashabiki na wadau wanaodai kuwa tabia ya wasanii kuiga filamu za Kinigeria imekithiri mno.

Msanii huyo, ambaye jina lake halisi ni Blandina Chagula ameenda mbali zaidi na kudai kuwa watu wanaangalia mambo mabaya tu kwa kila wanachofanya wasanii wa Tanzania na hata wafanye zuri gani halionekani.

Johari amesisitiza kuwa watu wanaowaponda hawaelewi wanachozungumza na wala hawaangalii mara mbili juhudi zinazofanywa na wahusika.

"Nashangaa watu wanaosema tunaiga, kila kitu kikifanyika utasikia tu wale wameiga, huku ni kukatishana tamaa," anasema msanii huyo aliyezaliwa mkoani Shinyanga Julai 27,1983.

"Kila mtu anaangalia tu kukosoa...Wanasema tunaiga Nigeria lakini mwisho wa siku ukiangalia utagundua kuwa hawana hoja kwavile mazingira ya Kiafrika yanafanana, matatizo ya jamii ya Nigeria na Tanzania ni sawa kwa kiasi kikubwa.

"Ukiigiza kama tajiri lazima utakuwa na nyumba nzuri, gari zuri kama lile la msanii wa Nigeria au Ghana hatutofautiani, huwezi kuigiza kama tajiri halafu anaishi kihasara.

"Lakini mimi nikiigizia kwenye ghorofa au gari kali hapa Dar es Salaam naonekana naiga kwa vile eti msanii fulani wa Nigeria alishaigizia mazingira kama yale, sasa mnataka tufanye nini?

"Lazima tubadilike na kukubali vitu vyetu, wale wenzetu wamepiga hatua kwavile wameanza taratibu. Tunajitahidi sana kuuvaa uhusika ili kufikisha ujumbe kwenye jamii yetu na kweli mimi sioni kama kuna mtu anaiga."

"Msitukosoe tu, tupongezeni tunapofanya vizuri, hapa tulipo ni mbali ingawa kuna baadhi yetu ambao wamekuwa wakijidhalilisha kwa kufanya mambo yasiyo ya kiungwana kwenye jamii.

"Kuna baadhi ya wasichana ambao wanaendekeza rushwa ya ngono lakini ukijaribu kuangalia hayo mambo wanajitakia tu wenyewe labda kwa kutojiamini, kutojielewa au ndio hulka ya mtu."

Johari anasema kuwa mwaka huu amepania kufanya kazi kubwa; "Nilitulia kidogo nikiwa najipanga kwa mambo mengine na mwaka huu nimepania sana kufanya kazi za kiwango cha juu zaidi ya hizo zinazofahamika."

"Huu ni mwaka wangu wa kazi na nitadhihirisha hilo kwa vitendo nitafanya kazi kama prodyuza na kwa upande mwingine kama msanii," anasema msanii huyo aliyeibukia kwenye kundi la maigizo la Kaole.

Akizungumzia msanii anayemkubali Johari anasema; "Mimi hakuna kama Irene Uwoya huyu msanii amefanya kazi nzuri sana hasa mwaka jana, ni mtu ambaye habahatishi."

"Anafanya kazi kwa mpangilio na anauvaa uhusika ipasavyo mpaka shabiki anasisimka kwa mfano angalia filamu kama 'Oprah','Peace of Mind' na 'Shakira' amefanya vizuri na mtu yoyote ambaye ameziangalia filamu hizo ataelewa nini ninachomaanisha acha tu tumpe sifa zake anastahili."

Johari amekuwa miongoni mwa wasanii wa kike wanaofanya vizuri katika tasnia ya filamu nchini kama ilivyo pia kwa wasanii kama Nora, Uwoya, Monalisa na wengineo.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3627