Sep 9, 2010, 9:31 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-03-08 17:09:00
Dully, Nay wamrudisha Sister P
Sister P
Na Festo Polea

SISTER P ameamua kushirikisha wasanii wenye majina makubwa katika ramani ya muziki nchini, ambao anaamini watamrudisha kwenye chati kimuziki kama miaka ya nyuma.

Msanii huyo amemshirikisha Nay wa Mitego kwenye wimbo, ambao utabeba albamu yake ya 'Nani Mkali' na anaamini atafanikiwa.

Mwingine aliyefanya naye ni Dully Sykes anayetamba na singo ya 'Shikide'. Dully atasikika kwenye singo ya 'Wapotezee' huku Mchizi Mox naye akiwa katika orodha ya wasanii watakaombeba.

Akizungumza na Mwanaspoti, Sister P anasema amewashirikisha wasanii hao ili kuleta chachu katika muziki wake na amekanusha madai kwamba anataka watu hao wambebe.

"Ninachofahamu ni kwamba ukiweka sauti mbalimbali katika muziki wako unaongeza ladha na inakuwa rahisi kuvutia mashabiki," anasema Sister P.

Anasema ukimya wake; "Unajua muda mrefu nilikuwa nchi za jirani Burundi na Rwanda pamoja na Congo huko nilipata ofa ndefu ya kuimba nikiwa na bendi."

Msanii huyo, ambaye anatarajia kuachia albamu yake Agosti mwaka huu na kusisitiza asingeweza kuacha ofa hiyo na kurudi
Bongo haraka. "Nilipenda kurudi nchini kuendelea na kazi zangu, lakini meneja aliyenipeleka huko alipenda uimbaji wangu na alinitaka nikae zaidi," anaongeza.

"Nilipofika nchini niliangalia uelekeo wa muziki kwa muda mfupi ndipo nikaamua kuingia studio kurekodi kibao cha 'Nani Mkali'.

Katika hatua nyingine, Sister P anashangazwa na suala la kushuka kwa haraka kwa baadhi ya nyimbo za muziki wa kizazi kipya, ambazo hupigwa kwa miezi kadhaa na kuchuja.

"Nashangaa kwa nini nyimbo za Kibongo husikika na kufa haraka, ni tofauti na nchi za wenzetu ambapo nyimbo husikika kwa muda mrefu." anasema.

Msanii huyo anaongeza kuwa jina lake linamsaidia kurekodi katika studio yoyote bure.

"Hata nikifulia kiasi gani, mimi ni staa ninaweza kurekodi popote bila kulipa fedha," anasema Sister P ambaye 'Anakuja Sister P' ni singo yake iliyong'ara.

Akizungumzia matarajio yake ya baadaye anasema anataka kujikita katika bendi kwani atapata faida zaidi.

"Mwaka huu, 2010, nataka mashabiki wasubiri kuona moto ninaokuja nao kwani nimerudi upya na sitaki kupoteza kazi zangu."
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3626