Sep 9, 2010, 9:33 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-03-06 04:52:00
Papic afanya usajili Simba
MICHAEL MOMBURI

FC LUPOPO inasita kumuuza mshambuliaji wao hatari Mumba Felix Sunzu kwa Simba, lakini kocha wa Yanga Kosta Papic amewaambia Simba; "Mkimsajili mtakuwa mmelamba dume."

Akizungumza na Mwanaspoti jana Ijumaa, Papic maarufu kwa jina la Clinton alisema Sunzu ni mchezaji mzuri ambaye hakuna klabu ambayo inaweza kumkataa.

"Simba wakimpata watakuwa wamelamba dume, wakitaka niwashauri kuhusu mshambuliaji huyo nitawaambia jibu moja; mchukueni haraka," alisema Papic aliyezikochi klabu tisa za Afrika tangu mwaka 2000.

"Lakini sidhani kama Sunzu anataka kucheza Afrika, viongozi wake wanasema anakwenda kufanya majaribio Ulaya hivi karibuni, sijui kama Simba wanaweza kumpata.

"Ila kama wakimpata itakuwa ni balaa, na kama wakija kwangu kutaka ushauri ni rahisi tu, wamsajili haraka," alisema
Papic ambaye ameomba kazi ya ukocha wa Taifa Stars.

Papic jana Ijumaa mchana alifanya kikao cha saa mbili na mfadhili wa klabu hiyo, Yusufu Manji na kuweka tofauti zao pembeni kwa muda.

Mumba ambaye ni Mzambia aliibua gumzo jijini Dar es Salaam baada ya kuinyanyasa Yanga katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika akiwa amevaa jezi namba 9, kitu kilichofanya baadhi ya viongozi wa Kamati ya Usajili ya Simba waanze kula naye sahani moja.

Lakini uongozi wa Lupopo kupitia kwa Katibu wake, Ilunga Lumbala uliiambia Mwanaspoti jijini Lubumbashi kuwa; "Mumba tumemnunua dola 50,000 (shilingi milioni 65) kwa AS Marsa ya Tunisia, kama Simba wanamtaka watupe dola 150,000 (sh.mil.180) chini ya hapo hapana, bado tunamhitaji."

"Simba wamezungumza na sisi lakini ukiangalia unaona kwamba hawataweza kumlipa mshahara ndio maana sisi tunataka kumuuza Ulaya tena kwa mkopo wa miaka miwili halafu arudi kwetu.

Hata hivyo, Sunzu alibanwa vilivyo katika mechi iliyofanyika Lubumbashi kwani alikuwa chini ya ulinzi mkali wa George Owino ambaye alifanya kazi kubwa katika mechi hiyo.

Lupopo iliitoa Yanga kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 4-2 huku Mumba ambaye anataka dola 7000 (sh.mil.9) tu asaini Simba akiwa ameifunga Yanga bao moja jijini Dar es Salaam.

Mumba amekuwa akilalamika kuona Simba ipo kimya wakati akiwa anataka kujiunga na kocha wake wa zamani, Patrick Phiri.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3623