OSWARD Morris wa Prisons amewaambia wenzake: "Komaeni tuifunge Toto African kwani mechi hii ndio itakayoamua maisha yetu.'
Prisons inashuka kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo Jumamosi kuivaa Toto African katika mchezo unaokutanisha timu zilizo katika hatari ya kushuka daraja.
Morris, ambaye ameichezea Prisons kwa miaka 14, alisema mchezo huo ni kama wa fainali na kwani ndio utatoa mustakabali wao wa kubaki kwenye ligi.
"Tukiishinda Toto African tutajiweka pazuri na tutapanga mikakati madhubuti ya kuhakikisha tunashinda mechi zote zilizobaki, lakini tukifungwa hali itakuwa ngumu."
Prisons ikishinda itafikisha pointi 20 na itasalia na mechi tatu, ambazo ikishinda itamaliza ligi na pointi 29 wakati Toto African inayokamata mkia ikiwa na pointi 13 ikiibuka na ushindi itakuwa na pointi 16, nayo itabakiza mechi tatu.