Sep 9, 2010, 9:29 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-03-05 16:47:00
Jela yampa kiwewe Lil Wayne
Wayne na mwanae
NEW YORK, MAREKANI

MWANAMUZIKI Lil Wayne, ametengeneza video nane kwa kipindi cha mwezi mmoja huku akisubiri kusikiliza hukumu yake, na inakadiriwa huenda akafungwa kwa mwaka mmoja jela.

Mwanamuziki huyo alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai, 2007 kwa kosa la kukutwa na silaha kinyume cha sheria na baada ya uchunguzi yakinifu, Lil Wayne alipatikana na hatia.

Na sasa mwanamuziki huyo anafahamu ataingia jela ndio maana ameamua kutoa video kadhaa, ambazo zitaendelea kutamba wakati akiwa 'lupango'.

Mwanamuziki huyo ameshirikiana na "Diddy" Combs, Rick Ross, Drake na Travis McCoy katika kukamilisha video hizo.

Lil Wayne amesema ana mpango wa kuachia albamu mpya itakayokwenda kwa jina la 'Tha Carter IV' mwanzoni mwa mwaka 2011.

Na katika hatua nyingine, hukumu ya mwanamuziki huyo iliyokuwa itolewe katikati ya wiki hii iliahirishwa baada ya kutokea kwa moto katika Mahakama ya New York.

Jaji Charles H. Solomon alikuwa akisubiriwa kutoa hukumu lakini mtafaruku wa moto ulimfanya aahirishe. Tarehe nyingine ya hukumu hiyo haijatangazwa.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3606