Sep 9, 2010, 9:38 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-03-02 11:20:00
Defoe awa mhubiri, aonya wachezaji
Mpachika mabao wa Tottenham, Jermain Defoe
LONDON, ENGLAND

MPACHIKA mabao wa Tottenham, Jermain Defoe amewataka wanasoka watulie na kuacha kufanya mambo ya ajabu, ambayo yanawavunjia heshima.

Mshambuliaji huyo amesema wakati umefika kwa wachezaji wa England kujichunguza tabia zao na kuachana na baadhi ya mambo yasiyofaa.

Defoe amesema kuwa wanasoka wanatakiwa kuonyesha heshima ndani na nje ya uwanja.

Defoe mwenye miaka, 27 aliongeza: "Wachezaji wanapaswa kufahamu kwamba wao ni kioo cha jamii. Ni jambo rahisi kwa mtoto wadogo kujifunza tabia mbaya za mchezaji fulani kwa kuwa anampenda mwanasoka husika.

"Ni kweli hata sisi ni binadamu wa kawaida, ambao tunaweza kufanya makosa, lakini tunatakiwa kuachana na makosa yanayoepukika.

"Wachezaji wanatakiwa kuwa makini kwa kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea fainali za Kombe la Dunia baadhi ya vyombo vya habari huibua skendo na kuwakosesha amani.

"Inakuwa ni vigumu kwa mchezaji mwenye kashfa kufanya vema katika fainali hizo hasa anapokutwa na skendo za ajabu," alisema.

Defoe pia alisema kuwa huwa hanywi pombe wala hajawahi kutumia dawa za kulevya.

"Tangu nikiwa mdogo nimekuwa nikijituma katika mazoezi na mama yangu amekuwa akiniambia kwamba nidhamu ndio mbinu pekee ya mafanikio."
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3602