Sep 9, 2010, 9:03 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-02-06 04:56:00
Wachezaji sita Simba wamchosha Phiri
Na Michael Momburi

KOCHA wa Simba, Patrick Phiri amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutobweteka na kelele Yanga lakini amekiri kuwa wachezaji sita majeruhi wanamvurugia mipango yake.

Mashabiki wa Yanga walifurahia juzi Jumatano baada ya Kagera Sugar kutibua rekodi ya Simba na kulazimisha timu hiyo kutoka sare ya bao 1-1 kwenye uwanja wa Kaitaba. Simba tangu kuanza kwa ligi ilikuwa haijapoteza mchezo wala kutoka sare.

Lakini Phiri amewaambia mashabiki wa Simba jana kwa njia ya simu kupitia Mwanaspoti kwamba: "Waachane na Yanga, ambao kushangilia Simba kuteleza ni kawaida, wanachopaswa kuangalia sasa ni kuongeza ushirikiano."

"Cha msingi kwetu sasa siyo rekodi ni kuhakikisha tunatimiza lengo la kutwaa ubingwa haraka iwezekanavyo, hayo mengine yatafuata na hilo litawezekana kama Simba kila mmoja akiwa na ushirikiano wa kweli.

"Wasiangalie nani anafanya nini. Timu inarejea Dar es Salaam Jumamosi (leo) na nina wachezaji kama sita ambao bado hali zao si nzuri lakini wanaendelea kupona taratibu.

"Nahitaji mchango wako sana kwenye timu lakini sina jinsi, majeruhi hao ni Hillary Echessa, Mohamed Banka, Mike Baraza, Uhuru Suleiman, Ulimboka Mwakingwe na Nico Nyagawa."

"Angalau Nico na Banka wanaweza kuwa wamepona mpaka mechi ijayo na Manyema lakini hawa wengine bado sina matumaini, uhakika ni mdogo sana lakini timu bado ipo imara kama kawaida.

"Lengo ni kushinda mechi zote zilizobaki na sare na Kagera haiwezi kutuathiri tunapanga mikakati mipya kwa vile tunahitaji pia kufikiria Kombe la Shirikisho."

"Lakini kwa ugumu tunaopata kwenye mechi za Ligi itakuwa ni maandalizi mazuri," aliongeza Phiri ambaye aliwahi kuwapa Simba ubingwa mwaka 2005.

Simba inayoongoza msimamo wa ligi ya Bara kwa pointi 43 itacheza na mshindi kati ya Lengthen ya Zimbabwe au AS Adema ya Madagascar kwenye hatua ya pili ya Shirikisho.

Ili kutwaa ubingwa wa Bara, Simba inapaswa kushinda mechi nne tu kuanzia sasa ambazo ni dhidi ya Manyema, Moro United, African Lyon na Mtibwa.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3508