Sep 9, 2010, 8:56 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-02-05 18:43:00
Kuwalipa waamuzi 15,000/- kwa siku ni kashfa
KWA wale wanaofuatilia soka kwa miaka mingi wanafahamu soka yetu ilikuwa juu katika miaka ya 1970 na 1980.

Timu yetu ya taifa ilikuwa moto wa kuotea mbali pale ilipotwaa Kombe la Chalenji mwaka 1974 ilifuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980.

Siri ya mafanikio hayo ilitokana na ukweli kuwa Chama cha soka cha wakati huo (FAT) kilikuwa na mipango mizuri ya kuendeleza soka kuanzia kwa yosso.

Kitu cha pili ambacho kinapuuzwa na Shirikisho la soka la Tanzania (TFF) ni kulikuwepo kwa waamuzi wa kiwango cha juu waliokuwa wanaheshimiwa na Shirikisho la soka la Kimataifa (Fifa) na Shirikisho la soka la Afrika (CAF).

Waamuzi walikuwa kama akina Gratian Matovu, Zuberi Bundala, Gwaza Mapunda, Mshindo Mkenyenge, Kassim Chona Bundala, Mohamed Nyama, Hafidh Ally, Abdallah Rajab, Said Ally, Dustan Daffa na Mussa Lyaunga.

Hawa walikuwa juu mno wakichezesha fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika na michuano mingine mbalimbali.

Wadau wa soka wamekuwa wakilalamikia katika siku za karibuni kuwa waamuzi wanachezesha ovyo lakini watachezesha vizuri vipi wakati wanalipwa kiasi cha sh. 15,000 kwa siku.

Nyumba ya wageni ya kawaida sio chini ya sh. 10,000 hadi 15,000, bado huyu bwana hajala kuanzia asubuhi hadi jioni.

Kibaya zaidi fedha hizi hazilipwi kwa wakati, ambapo mwamuzi anapochezesha ligi hata mikoani anatakiwa kuzifuata Dar es Salaam, ambapo anazungushwa mno na watu wa sekretarieti wa TFF.

Inashangaza wakubwa wa TFF wanawasumbua mno waamuzi halafu jamaa hawa ni mabingwa wa kukimbilia kwenye vyombo vya habari na kuwabeza `eti' wamevunja sheria 17 wakati wao wakijua ndio chanzo kwa sababu wanachezesha mechi wakiwa na ukata.

TFF inafanya ubabaishaji huu dhidi ya waamuzi wakati wao wanapokea mamilioni ya fedha za uendeshaji kutoka Vodacom, NMB, Serengeti, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na Fifa.

Bado hayo makato ya milangoni wanayoziminya klabu na makusanyo mbalimbali ya mechi za timu ya taifa, Taifa Stars.

TFF inapaswa kujisafisha na mambo haya mawili, ambapo ipandishe mara moja malipo ya waamuzi na pili maafisa wake waache ubabaishaji na walipe madai ya waamuzi mara moja.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3503