Sep 9, 2010, 9:08 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-02-06 05:41:00
Msolla: Kocha wa Drogba anatufaa
Na Michael Momburi

PROFESA Mshindo Msolla amesema kuwa kushindwa kwa Ivory Coast ya Didier Drogba kutwaa ubingwa kwenye fainali za Afrika nchini Angola hakumaanishi kwamba kocha wake Vahid Halilhodzic hafai kuinoa Taifa Stars.

Halilhodzic ni kati ya makocha wenye chati kubwa duniani, ambapo alikuwa mchezaji wa zamani wa Yugoslavia wakati huo taifa lake la asili la Bosnia-Herzegovina likiwa chini yake na kukipiga kwenye fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1982 nchini Hispania.

Pia alipata kuzinoa klabu za Ufaransa PSG, Rennes na Lille aliyoisaidia kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa wa Ulaya kabla ya kupewa jukumu la kuinoa Ivory Coast.

Msolla ambaye ni kocha wa zamani wa Stars na Reli ya Morogoro, ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Vahid raia wa Bosnia na Ufaransa kukiri kuwa akitakiwa kuomba kazi hiyo atafanya hivyo haraka.

"Unajua mtu akiangalia atasema kwamba yule kocha hafai kwavile hajatwaa Kombe la Afrika lakini mkumbuke ameipeleka timu kombe la Dunia,"alieleza Msolla, ambaye aliwahi pia kuifundisha Reli ya Morogoro.

"Hatua aliyopiga inaonyesha kuwa ana sifa stahili mi naona kocha yoyote ambaye ameipeleka timu Kombe la Dunia anatufaa, Ivory Coast kushindwa kutwaa ubingwa inachanganyiwa sana na wale wachezaji wa nje.

"Wale wachezaji wengi wao hawajitumi sana kwenye majukumu ya Kitaifa kwavile wanathamini zaidi klabu zao Ulaya, utashangaa akifanya kazi na wachezaji wa hapa atakwenda mbali zaidi ya hapa alipo.

"Hawa wetu wanajituma zaidi ya hao mastaa, mi nadhani yule pia anafaa," aliongeza Msolla, ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uhamasishaji ya serikali ya kuhimiza Kampeni ya Kilimo Kwanza.

Tayari makocha toka nchini za Ufaransa, Venezuela na Uingereza wameomba kazi hiyo ya Stars huku mkataba wa kocha wa sasa Marcio Maximo ukiisha Juni.

Shirikisho la soka la Tanzania(TFF) bado halijaweka hadharani vigezo vya kocha anayetakiwa lakini habari za ndani zinadai lazima awe toka barani Ulaya na ameifikisha timu ya taifa kwenye Kombe la Dunia au Fainali za Mataifa ya Afrika.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3502