Sep 9, 2010, 9:10 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-02-05 18:25:00
Papic tuambie ukweli, si kutafuta sababu
Papic
Na Andrew Kingamkono
"HATUNA uwezo wa kuifunga Al Ahly hata kama tutafanya kila kitu kwa sababu ya kiwango cha wachezaji wangu, hawalingani hata kidogo na nyota wa Mabingwa hao wa Ligi ya Mabingwa Afrika," hiyo ilikuwa kauli ya kocha Dusan Kondic wakati Yanga ikijiandaa kucheza mechi yake ya kwanza jijini Cairo mwaka jana.

Kauli hiyo ilipigwa vikali na viongozi wa Yanga wakiongozwa na Mwenyekiti wao,Iman Madega pamoja wanachama na mashabiki kwa kusema kocha huyo amepanga kuuza mchezo huo.

Naamini kikubwa kilichofanya viongozi hao na mashabiki wa timu hii kumpiga Kondic ni kujiamini zaidi kwa kiwango cha klabu yao, ambayo ilikuwa imechukuwa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania kwa mara ya pili mfululizo tena wakiwa na mechi mkononi.

Lakini Mungu amfichi mnafiki ukweli ulithibitishwa vizuri kwenye Uwanja wa Taifa ambako Watanzania walishudia Yanga wakichezeshwa kama watoto wadogo na miamba hiyo ya Misri na kuchabangwa kwa jumla ya mabao 4-0, huku kila moja akitoka uwanjani akisema kweli Kondic alisema ukweli hawa jamaa hatuwawezi.

Mwishoni mwa mwaka jana Kondic alitimuliwa na kupewa nafasi yake Mserbia mwenzake Kostadin Papic kukiongoza kikosi cha mabingwa wao watetezi ambao msimu huu watakuwa wakitegemea miujiza kutetea ubingwa wao mbele ya Simba wanaoongoza ligi hiyo kwa pointi 42 na wakisubiri ushindi wa mechi tatu kutangazwa wafalme wapya.

Kocha Papic amegundua kuwa nafasi yake ya kupata ubingwa wa ligi ni mgumu hivyo taratibu ameanza kuelekeza mawazo na hisia zake zote kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Lupopo utakaochezwa jijini Dar es Salaam Februari 13, kabla ya mechi ya marudiano itayochezwa DR Congo kwa lengo ya kuinusuru Yanga isitolewa kwenye hatua za awali.

Taswira inamuunga mkono kwa asilimia mia kwani tumechoka kuona timu zetu zikitolewa kwenye hatua za awali kila zinaposhiriki katika michuano hii ya Afrika.

Lakini ni nimepatwa na hofu moja kubwa na kujiuliza je ni nani aliyekuja na wazo la kushangaza la kutaka Yanga isogezewe mbele mechi yao ya Ligi dhidi ya Mtibwa ili wapate muda mrefu wa kujiandaa na mchezo wake huo dhidi ya Wakongo hao ambao ni mabingwa wa nchi hiyo waliowazidi kete TP Mazembe, mabingwa wa Afrika.

Ni jambo la ajabu kabisa ambalo sikutegemea viongozi wa klabu kubwa kama Yanga kuomba kwa TFF kusogezwe mbele kwa mechi wakati wao ndio walikuwa mstari wa mbele kumpinga kocha Marcio Maximo anapowakata wachezaji wao kwa muda kwa ajili ya maandalizi ya Taifa Stars.

Hivi kwa mfano Yanga ingekuwa inacheza kwenye ligi ya England ambako klabu zake zinacheza mechi si chini ya tatu ambazo zina upinzani mkubwa huku wakiwa na mechi za Ligi ya Mabingwa wangeomba mara ngapi kusogezwa mbele kwa ratiba yao ya ligi.

Nadhani Yanga walipaswa kuifurahia ratiba hii dhidi ya Mtibwa na kutumia mchezo huu kama sehemu ya mazoezi yao kabla ya mechi ya Ligi ya Mabingwa kwa sababu wachezaji wao watakuwa kwenye hali nzuri zaidi kimchezo.

Kwa wachezaji wetu ambao kwa mwaka wanacheza mechi mbili kubwa zenye upinzani na ushindani wa kweli ambazo ni zile za Simba dhidi Yanga kwa mujibu wa kocha Maximo nadhani kucheza kwa mechi mfululizo za ligi na kujifunza kusafiri kila wiki kutawasawaidia kuwakabili vizuri Lupopo ambao wanaonekana kuwa ni wapinzani wa kweli.

Taswira inafikiri viongozi wa Yanga na kocha Papic wanapaswa kuwa wa wazi kuhusu kiwango cha wachezaji wao na si kutafuta sababu zisizo na msingi kwamba TFF imewanyima muda wa kutosha wa kufanya mazoezi.

Sababu kubwa ya kubadilika kwa ratiba ya ligi ni kutokana na kuonekana timu za Tanzania zinashindwa kufanya vizuri kwenye michuano hii ya Afrika kwa sababu timu zetu ziliingia katika fainali hizi wakati ligi ikiwa imemalizika siku nyingi na kipindi ambacho walikuwa wakifanya usajili hivyo iliwawia vigumu kushindana.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3494