Sep 9, 2010, 9:13 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-02-01 19:21:00
Chelsea yamkingia kifua Terry
LONDON, England
LICHA ya John Terry kukabiliwa na madai ya kutembea na mke wa Wayne Bridge, Chelsea imesema itampa ushirikiano katika kipindi hiki kigumu.

Habari kutoka Chelsea zinasema mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abramovich alimwita Terry na kumwambia klabu ipo pamoja naye katika kipindi hicho kigumu.

Kumekuwa vielelezo vya wazi vinavyothibitisha kwamba Terry alilala na aliyekuwa mke wa Bridge aitwaye Vanessa Perroncel, lakini Abramovich anaona kuwa hakuna sababu ya kumchukulia hatua za kinidhamu mchezaji huyo.

Mtu mmoja wa karibu na Abramovich alisema: "Roman alimwambia John kuwa asiwe na wasiwasi kwani Chelsea haitamtupa katika wakati huo mgumu.
"Nadhani anahitaji kutulizwa katika kipindi hiki kigumu.

"Ukweli ni kwamba Terry hajavunja sheria. Jambo la msingi ni kuhakikisha anashughulikia suala hilo mpaka litakapomalizika.

"Ni mtu anayeheshimika katika kikosi, ni mmoja kati ya wanafamilia wa Chelsea."

Wiki hii, Terry alifanya mazoezi na wachezaji wenzake kama kawaida na hali ilikuwa shwari uwanjani, hakukuwa na minong'ono yoyote.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3485