RIO DE JANEIRO, Brazil
MSHAMBULIAJI wa Brazil, Adriano alifunga mabao matatu 'hat-trick' kuiongoza Flamengo kushinda 5-3 dhidi ya Fluminense.
Baada ya kuongoza kwa mabao 3-1 kwenye kipindi cha kwanza huku beki Alvaro akiwa ametolewa kwa kadi nyekundu dakika 63, Flamengo iliendelea kutawala mchezo huo kwenye uwanja wa Maracana huku washambuliaji wake Adriano na Vagner Love wakionyesha kiwango cha kuvutia.
"Tunacheza kwa kusaidiana, wote tuna malengo yanayofanana kupata nafasi ya kucheza Kombe la Dunia," alisema Adriano.
Fluminense ilipata mabao yake mawili mwanzoni kupitia kwa Andre na Dario Conca walionekana kuelewana vizuri bila ya kuwepo kwa mshambuliaji wao tegemeo Fred aliyekuwa majeruhi.