Sep 9, 2010, 9:00 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-02-02 02:08:00
Wakati kwa soka la mikoani kufufuliwa
SIMBA imeendeleza ubabe wake kwenye Ligi Kuu ya soka ya Tanzania Bara baada ya kuilaza Toto African ya Mwanza 2-0 kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Kwa matokeo hayo, Simba ilizidi kupaa kwenye msimamo wa ligi hiyo kutokana na kufikisha pointi 42 na kuzidi kuuchungulia ubingwa.

Mchezo huo, ulikuwa mkali kutokana na uongozi wa mkoa wa Mwanza chini ya Abbas Kandoro kupania kuhakikisha Toto inashinda ili kutoshuka daraja.

Ilikuwa jambo la kushangaza kuwa uongozi wa Mwanza uliweka nguvu kubwa katika kushinda mchezo huo, ili kuisaidia Toto wakati huu iko taabani kwenye msimamo wa ligi.

Pia umati mkubwa wa mashabiki wa Mwanza ulikuwa umejitokeza katika kuishangilia timu hiyo kuondoka na ushindi.

Funzo kubwa linajitokeza hapa ni kuwa kuna haja ya watu wa mikoani kukusanya nguvu zao na kuinua msisimko wa soka la huko.

Hivi sasa sio siri tena, mashabiki wa soka wa mikoani wamehamishia ushabiki wao kwenye soka la nje na hasa Ligi Kuu ya England.

Hakuna wa kuwalaumu kutokana na ukweli kuwa ligi za mikoa zimepoteza utamu na kufanya mashabiki wa mikoani kukosa burudani.

Nani atasahau timu kama AICC, Ndovu, Kiltex na Mulbadaw (Arusha), CDA, Kurugenzi na Waziri Mkuu (Dodoma), Mseto, Tumbaku, Reli (Morogoro) na Lipuli na African Wanderers za Iringa.

Imefika wakati kwa watu wa mikoani kukusanya nguvu zao kama ilivyokuwa zamani kwa timu za Mseto, Coastal Union ya Tanga, Pamba ya Mwanza, Majimaji ya Songea na Tukuyu Stars zilivyokuwa zinapigana vikumbo na Simba na Yanga kuwania ubingwa.

Hilo linawezekana ikiwa kuna dhamira ya dhati kutoka kwa wahusika mbona iliwezekana kwa timu hizi kunyakua ubingwa za Mseto (1975), Majimaji (1985, 1986) na Pamba (1990).
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3478