Sep 9, 2010, 9:06 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2010-01-25 19:14:00
Sarah Kais awashushua wenzake
Sarah
Na Festo Polea

SARAH Kais amewashushua wasanii wa muziki nchini na kuwaambia kuwa kama wakiendelea na masihara na kutokuwa makini ni ngumu kushindana kwenye soko la kimataifa.

Msanii huyo, ambaye mwaka huu anaonekana kujipanga kikamilifu amewaambia wasanii hao wenzake kuwa wasipobadilika mastaa wa kigeni watazidi kutawala katika tuzo zote.

Anasema kuwa wasanii wengi ni woga kutumia fedha na wanaogopa kuwekeza ndio maana kila mwaka wamekuwa wakibaki hapo hapo walipo bila mabadiliko yoyote huku wale wa nje wakizidi kuchanja mbuga na kutawala mpaka soko la Bongo.

Sarah anasema wasanii wa Tanzania wanashindwa kunyakua tuzo na hawatazinyakua hata miaka kumi ijayo kwa kuwa wanaogopa kupata hasara katika kuwekeza kwenye muziki hivyo hujikuta wakikurupuka na kuigeuza sanaa hiyo kuwa kiburudisho badala ya kazi.

"Hatupo makini na kwa njia hii hatufiki popote tutazidi kuwa hapahapa tulipo, unakuta msanii analipia video anafanya yote kwa siku moja, hivi amejipanga muda gani, hayo mavazi atayapanga vipi matukio ya wimbo wake ameyafanyia mazoezi muda gani."

"Namna hii unategemea utoe kitu gani bora ambacho kitaonyesha uko makini, kwanini usifanye kazi taratibu watu waone kwamba uko makini na unaithamini kazi yako inayokuweka mjini, muziki si sehemu ya kutafutia sifa ni kazi hii."

"Wasanii kama Nameless, Amani, DiBanj wamejipanga, wamewekeza muda mrefu katika muziki kuanzia nyimbo hadi video na wanajua kuwa fedha nyingi zinapotea lakini zitajilipa baadaye ambapo kwa sasa wananufaika nazo katika tuzo mbalimbali."

Sarah anayevuma na wimbo wa "Mtimanyongo" anasisitiza kuwa wasanii wengi nchini huenda kwa watengeneza picha za video na kutaka kupigiwa picha hizo kwa siku moja kwa lengo la kuuza sura bila kujali ubora wa kazi yake na malengo ya baadaye.

Katika harakati za kujitanua kimafanikio, Sarah amejiwekea malengo kadhaa ikiwa ni pamoja na kuzindua kampuni yake binafsi itakayokuwa na kazi ya kuendeleza wasanii mbalimbali wasiojiweza katika fani mbalimbali.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=3443