LONDON, England
KOCHA wa Chelsea, Carlo Ancelotti amesema kikosi chake kinatakiwa kujiimarisha vema ili kuepuka kipigo kingine.
Timu hiyo ilichapwa mabao 2-1 na Aston Villa huku wauaji wakiwa Richard Dunne na James Collins. Bao la kwanza la Chelsea lilifungwa na Didier Drogba.
"Tumekosa amani kwa sababu tulicheza vema na kupoteza mchezo, hatukuwa na sababu ya kupoteza mechi hiyo," alisema Ancelotti.
"Mtu huwezi kupata maumivu makali kama timu yako imecheza chini ya kiwango na kufungwa, Villa walijitahidi, lakini kiwango cha Chelsea kilikuwa kikubwa zaidi.”
"Katika mechi zinazokuja tunatakiwa kujituma zaidi, naamini jitihada kubwa huzaa matunda mazuri.”
"Tulipofungwa, tuliumia sana, lakini baada ya muda kidogo wachezaji walisahau maumivu na kufikiria mechi nyingine," alisema.