Sep 9, 2010, 9:21 am TFF UEFA FIFA Yahoo Sport CAF Staff Mail Premier League English News Spoti Majuu
 
 
 
 
 
 
 
 

 

Imewekwa:: 2009-10-09 18:58:00
Argentina ni kufa au kupona
Maradona ambaye ni kocha wa Argentina
LONDON, England

"MWANAUME mbaya", Nolberto Solano anatarajia kukiongoza kikosi cha Peru katika kumuongezea hasira kocha wa Argentina, Diego Maradona katika mechi ya kufuzu ya fainali za Kombe la Dunia 2010.

"Nataka kuonyesha soka safi dhidi ya Argentina na kuweka historia kama ile ya wacheza filamu wakorofi, lengo ni kuiua timu kubwa duniani," alisema nahodha huyo wa Peru wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Aliongeza kuwa kama Argentina ikitinga katika fainali hizo zitakazofanyika nchini Afrika Kusini itakuwa ni kwa bahati sana, watakumbuka 'muziki waliouchezea' katika mechi za kufuzu.

Argentina, inashika nafasi ya tano katika Kundi la Amerika Kusini na itahitaji kuifunga Peru na baadaye (Jumatano) Uruguay ili angalau kuingia katika mechi za mtoano na mshindi wa nne wa Kundi la Amerika ya Kati na Kaskazini
(CONCACAF).

Nayo Serbia inaweza kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2010 na kuipiku Ufaransa iliyoshika nafasi ya pili katika fainali za mwaka 2006 kama ikiishinda Romania, leo Jumamosi.

Ujerumani nayo itakuwa ikisaka nafasi wakati itakapokwaana na Russia katika mechi ya kundi la nne itakayochezwa jijini
Moscow.

Pointi tatu katika mechi dhidi ya Sweden zinaweza kuifanya Denmark itue Afrika Kusini wakati ushindi kwa kikosi cha Sweden utamanaisha kuwa Ureno yenye mchezaji nyota Cristiano Ronaldo itaangalia fainali hizo kupitia runinga iwapo itashindwa kuifunga Hungary.

Serbia, ambayo inaongoza Kundi la Saba ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza mechi nane inahitaji ushindi mmoja katika mechi mbili zilizobaki na itacheza nyumbani na Romania kisha Jumatano ijayo itacheza na Lithuania.

Ufaransa inayoshika nafasi ya pili haina hata uhakika wa kucheza mechi za mtoano mwezi Novemba kwa kuwa Austria iliyo nyuma yao kwa pointi nne inaweza kupunguza umbali na kuwa nyuma kwa pointi moja. Ufaransa itapambana na Visiwa vya Faroe.

Ujerumani, ambayo itaingia uwanjani bila kuwepo kwa wachezaji pacha wa VfB Stuttgart, Serdar Tasci na Sami Khedira, iko juu ya Russia kwa pointi moja na itahitaji ushindi ili kuungana na vikosi vya Hispania na England katika fainali hizo zitakazochezwa Afrika kwa mara ya kwanza.

England inatarajia kucheza mechi na Ukraine huku Hispania ikicheza na Armenia katika mechi za kukamilisha ratiba.

Russia imeshapata nafasi katika hatua ya mtoano lakini itatakiwa kuvifunga vikosi vya Ujerumani, leo Jumamosi na Azerbaijan Jumatano ijayo ili kujihakikishia nafasi ya moja kwa moja.

Kazi ni nyepesi kwa vinara wa Kundi la Tatu; Slovakia ambayo inatafuta pointi moja katika mechi ya nyumbani dhidi ya kikosi kinachoshika nafasi ya pili cha Slovenia.

Kocha wa Italia, Marcello Lippi ameviudhi vyombo vya habari kwa kushindwa kumwita Antonio Cassano lakini yote yatasahaulika kama timu hiyo itapata pointi jijini Dublin katika mechi dhidi ya Ireland.

Denmark, katika Kundi la Kwanza itakuwa na hasira ya kushindwa kuingia fainali za Mataifa ya Afrika 2008, lakini itatakiwa kuiumiza Sweden yenye wachezaji machachari akiwemo Zlatan Ibrahimovic jijini Copenhagen.

Ureno iliyo nyuma ya Sweden kwa pointi mbili haitakuwa tayari kupoteza pointi katika uwanja wa nyumbani mbele ya Hungary na kikosi hicho kitakuwa na amani zaidi kwa kuwa Ronaldo amepona.

Vinara wa Kundi la Pili Uswisi, ambao watasafiri kwenda Luxembourg wakiwa juu kwa pointi tatu dhidi ya Ugiriki na Latvia watatakiwa kufanya vema wakati wakisubiri matokeo kati ya Ugiriki na Latvia huko Athens.
Toa Maoni Chapisha(Print) Facebook Tuma kwa rafiki
Habari Zingine
Phiri hana shida, Mgosi, Kanoni waibukia Tanga
Mkenya aipa Simba mambo mawili
Henry arudi Norway majeruhi
Kiungo Yanga mambo mazuri
Mafisango atunisha msuli,aigunia Simba Tanga
Humoud azua tafrani Simba
Wabongo wamrudisha Mariga Dar
Rage aidai Mwanaspoti Sh. bilioni moja
Jabulani kumi zaisisimua Simba
Kipa Yanga aingilia anga za Kaseja
 
 
 
 
 
© Mwananchi Communications Ltd:2007-2010:Started October 1,2007http://www.mwanaspoti.co.tz/readnewzt_sp.php?id=2626